Home / Habari Za Kitaifa (page 141)

Habari Za Kitaifa

MTOTO WA MIAKA 11‘ATUNUKIWA’ PhD

WAHITIMU, viongozi na wageni waliohudhuria Mahafali ya 32 ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro, waliingiwa na simanzi wakati mtoto, Tamar Aaron Mbogho (11), alipojitokeza na kupokea Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD), akimwakilisha mama yake Swai Sophia Faustin ambaye alifariki dunia miezi sita kabla ya kufika …

Read More »

MAGUFULI AWEKA HISTORI JWTZ

RAIS John Magufuli ametunuku Kamisheni kwa maofisa wanafunzi 194 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 59/15 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa maofisa wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni nje ya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo …

Read More »

Majaliwa ambana Mwakyembe

Mwandishi Maalum WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kumpa maelezo sababu za Tanzania kutokukamilisha Mkataba wa Mawakili wa Afrika Mashariki kutambuana katika utendaji wao. Alitoa agizo hilo jana wakati akimwakilisha Rais John Magufuli katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa …

Read More »

MAGUFULI AMPONGEZA MAKONDA

RAIS John Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa juhudi za kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Magufuli ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na Mkuu huyo wa Mkoa huo kwa njia ya simu wakati Makonda akiendelea na mkutano wa hadhara katika eneo la Mbezi …

Read More »

TANESCO YAPATA FAIDA BILIONI 449/-

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema katika hesabu za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka 2014/2015, zimeonesha kwamba, limepata faida ghafi ya Sh bilioni 186 na ya uendeshaji ya Sh bilioni 263. Faida hiyo iliyopatikana kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu, inatokana na shirika hilo kuwa …

Read More »

VETA KUIMARISHWA KUENDELEZA VIWANDA

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya ufundi stadi nchini (VETA) ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi soko la ajira, hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitakavyojengwa nchini. Ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo mkoani Arusha …

Read More »

ATCL DAR- KIGOMA.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani akiwaaga viongozi na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mkoani Kigoma baada ya kuzindua safari za ndege aina ya Bombardier Q400 kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano …

Read More »

WAKURUGENZI 5 ATCL KUNG’OLEW

BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imeeleza kuongezeka kwa makusanyo ya shirika hilo katika kipindi kifupi cha uendeshaji wake kutokana na kudhibitiwa kwa mapato na matumizi. Aidha bodi hiyo imeagiza kuwaondoa wakurugenzi watano na baadhi ya mameneja katika nafasi zao kwa kuwa wengi wao wana viwango …

Read More »

90% WANAOTIBIWA MOYO MUHIMBILI WANAPONA.

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeendelea kuonesha maajabu katika matibabu ya moyo ambapo ndani ya wiki moja iliyopita imeweza kufanya matibabu ya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 17 kwa ufanisi mkubwa na kuandika historia ya aina yake. Madaktari bingwa wa taasisi hiyo iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya …

Read More »

WAZIRI AAGIZA FEDHA ZA TASAF ZIRUDISHWE

SERIKALI imeagiza fedha zilizotolewa kwa kaya zisizokuwa na sifa katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaofanywa kwa uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kurejeshwa. Aidha imetoa siku 14 kuanzia jana kwa wakuu wa mikoa kufikisha taarifa ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya watendaji waliojihusisha na upotevu huo wa fedha. …

Read More »