Home / Habari Za Kitaifa (page 30)

Habari Za Kitaifa

Kortini akidai kachero wa usalama anamfuatilia Tundu Lissu

MKAZI wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mbutusyo Mwakihaba (40) amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kuchapisha maneno ya uongo kuhusu kachero wa usalama wa Taifa kumchunguza Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayepatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya. Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa, …

Read More »

Polisi Arusha yazuia mikutano ya Lema

MIKUTANO miwili ya hadhara iliyokuwa ifanyike jijini Arusha jana na leo na kuhutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema imepigwa marufuku. Lema jana alipaswa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la Soko Kuu katika Kata ya Kati na mwingine ulipangwa kufanyika leo katika Kata ya Kimandolu, lakini …

Read More »

Majambazi wapora msikitini, wamjeruhi mlinzi kwa panga

WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wamevamia Msikiti Mkuu wa Ijumaa ulioko Kata ya Igunga Mjini wilayani hapa mkoani Tabora, kisha kumjeruhi mlinzi na kupora baadhi ya vitu ikiwemo vitabu vya dini ya Kiislamu. Mlinzi aliyejeruhiwa ni Juma Mussa (55), mkazi wa Mtaa wa Nkokoto kata ya Igunga ambaye amelazwa katika …

Read More »

‘Wasiojulikana’ wamuua Ofisa Tarafa

OFISA Tarafa wa Lupiro wilayani Ulanga Mkoa wa Morogo, Beno Polisi ameuawa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira alilithibitishia HabariLeo jana kuwa watu hao walimvamia Ofisa Tarafa huyo nyumbani kwake muda wa saa tatu na nusu usiku na kumshambulia kwa …

Read More »

120,000 huongezeka Dar kila mwaka

JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa miji mikubwa nchini inayoathiriwa na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Ili kukabiliana na tatizo hilo Tanzania inahitaji dola za Marekani milioni 500 kila mwaka kwa ajili ya kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri miji mikubwa …

Read More »

JPM atoa mil 260/- nyumba zilizoungua

RAIS John Magufuli ametoa Sh milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za polisi jijini Arusha, ikiwa ni msaada kwa jeshi hilo baada ya familia 45 kukosa mahali pa kuishi kutokana na nyumba 15 walizokuwa wakiishi kuungua moto juzi. Aidha, Rais amemwagiza Mkuu wa Kitengo cha Wakala wa Majengo …

Read More »

Polisi wapewa kompyuta 20, pikipiki 10

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi vitendea kazi kwa jeshi la polisi zikiwemo kompyuta ambazo zitasambazwa katika vituo vya polisi 20 vya mkoa huo. Mbali na kompyuta hizo, Makonda pia amekabidhi pikipiki 10 kwa ajili ya kikosi cha usalama barabarani na baiskeli 200 ambazo zitawasaidia kufanya …

Read More »

TCRA yatoa leseni vituo 32 vya TV

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa leseni kwa vituo 32 vya televisheni hapa nchini. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alitaja idadi ya vituo hivyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Vijijini, Martin Msuha (CCM). Msuha alitaka kujua kuna vituo vingapi vinarusha matangazo kwa njia …

Read More »