Home / Habari Za Kitaifa (page 4)

Habari Za Kitaifa

Mwita Waitara ajiunga na CCM

Mwita Waitara

Mbunge wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania Mwita Waitara amejiunga na chama tawala nchini humo CCM. Waitara kutoka eneo bunge la Ukonga alitangaza uamuzi huo katika mkutano na vyombo vya habari mapema Jumamosi. Katika mkutano huo ulioandaliwa na katibu wa CCM anayesimamia maswala ya umma Humphery Polepole, kiongozi …

Read More »

Mwalimu Mkuu Adaiwa Kumjaza Mimba Mwanafunzi

Jeshi la Polisi wilayani Nkasi mkoani Rukwa linamsaka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, Eradi Kapyela anayedaiwa kuikimbia shule yake akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14 . Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi ipo katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika …

Read More »

Madiwani Chadema, CUF Wanaswa Baa

Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mmoja wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakidaiwa kupokea rushwa ya Sh milioni tatu ili kumpitisha mzabuni wa ujenzi wa soko la kisasa la …

Read More »

Lugola: Nataka Mtambo au Bil 2/= NIDA

Lugola

Serikali imetoa wiki mbili kwa Kampuni ya Iris Corporation Berhard ya Malaysia, kurudisha Sh bilioni 32 zilizotolewa au kuleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi za Vitambulisho vya Taifa baada ya kushindwa kutekeleza jambo hilo kwa miaka mitatu sasa. Pia kampuni saba zilizokuwa katika mradi wa vitambulisho vya taifa zimeitwa, kujieleza …

Read More »

Uchimbaji Wa Madini Ya Kaolin Wasitishwa

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameiagiza Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya RAK inayochimba madini ya kaolin yanayotumika kutengeneza marumaru kusimamisha shughuli zake kwa siku mbili ili kujiridhisha thamani halisi ya madini hayo. Nyongo ametoa agioz hilo alipofanya ziara katika Kijiji cha Kimani wilayani Kisarawe mkoani Pwani, ambalo ni …

Read More »

Wamkubali Magufuli

rais magufuli

Wasomi, wanasiasa, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida, wamezungumzia gawio la Sh bilioni 736.36 lililotolewa kwa serikali kupitia taasisi, kampuni, mashirika na wakala wake kwa mwaka wa 2017/18. Juzi Rais John Magufuli alipokea mfano wa hundi za gawio la kiasi hicho cha fedha, licha ya kupongeza, aliagiza mashirika ambayo hayajatoa gawio, …

Read More »

TANZANIA, KOREA KUSINI ZAONDOA VIZA

SERIKALI ya Korea Kusini na ya Tanzania zimeingia makubaliano ya kidiplomasia kuondoa viza kati ya nchi hizo mbili kwa watu wenye hati za kusafiria za diplomasia na zile za utumishi. Makubaliano hayo yasainiwa leo mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu wa Korea, Lee Nak-Yon. Makubaliano …

Read More »