Home / Habari Za Kitaifa (page 5)

Habari Za Kitaifa

TCU, NACTE WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameagiza taasisi za elimu ya juu zilizohakikiwa na kubainika kuwa zina upungufu mbalimbali, zirekebishe kasoro hizo mapema iwezekanavyo. Amesema zinatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia maelekezo ya mamlaka husika zinazosimamia ubora wa elimu ya juu, yaani Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania …

Read More »

TALAKA 286 ZATOLEWA KWA MIEZI MITATU

TAKWIMU zinaonesha Zanzibar bado inakabiliwa na ongezeko la talaka na hivyo kuchangia kuwepo kwa idadi kubwa ya watoto wanaokosa ya malezi ya baba na mama. Mwanaharakati na mtafiti kutoka Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa), Salma Maulid amesema Januari hadi Machi mwaka huu, talaka 286 zilitolewa Mahakama ya Kadhi. Amesema hayo …

Read More »

VIWANJA 21,000 KUUZWA KWA WENYE KIPATO KIDOGO

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma itapima viwanja 21,000 kwa ajili ya watu wa kawaida na wale wa kipato cha chini. Mkurugenzi wa Jiji hilo, Godwin Kunambi amewaeleza waandishi wa habai kuwa, mpango wa Jiji ni kuhakikisha watu wote wenye kipato kikubwa na kipato wanapata fursa ya kuishi jijini humo. Kunambi …

Read More »

Marekani Yaguswa na Ujio Wa Dreamliner

Ubalozi wa Marekani nchini umesema unaunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika ununuzi wa ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner katika kukuza uchumi wa taifa. Katika kuonesha kwa vitendo kuunga mkono juhudi hizo za serikali ya Rais John Magufuli, imesema kwamba Julai 29, mwaka huu, itatumia ndege hiyo …

Read More »

Zabibu Dhahabu ya Dodoma

zabibu

KITUO cha Utafiti cha Makutupora (TARI) jijini Dodoma kimepewa Sh milioni 400 kwa ajili ya kupanua huduma za utafiti wa zao la zabibu mkoani humo na katika maeneo mengine nchini. Kituo hicho kinachofanya kazi chini ya Wizara ya Kilimo, ni maalumu kwa ajili ya utafiti wa zao zabibu, aina zake, …

Read More »

Waziri Mkuu: Tuenzi Utamaduni, Tutunze Mazingira

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa, mawaziri na wabunge wawahamishe Watanzania kuendeleza utamaduni wao nchini. ‘ Ametoa mwito huo wakati akizungumza na wazee na wananchi wa Makunduchi baada ya kushuhudia maadhimisho ya sikukuu ya Mwaka-Kogwa yaliyofanyika Makunduchi, wilaya ya Kusini, mkoa wa Kusini Unguja. “Mawaziri tuna dhamana ya kuwahamasisha Watanzania …

Read More »

Zawadi ya Magufuli kwa Obama

zawadi ya magufuli kwa obma

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama amekuwa kwenye ziara barani Afrika ambapo sehemu ya ziara hiyo imekuwa ya faragha na nyingine ya wazi. Kuna mambo mengi sana ambayo ameyatenda na kuyasema wakati wa ziara hiyo yake ya kwanza Afrika tangu alipostaafu urais mapema mwaka jana. Bw Obama alianza ziara yake …

Read More »

Moto Katika Hifadhi ya Serengeti

nyumbu wa serengeti

Serikali ya Tanzania imekanusha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuwa mamlaka za hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania zimefanya hujuma kuchoma moto eneo la hifadhi ili kuzuia nyumbu kuvuka kuelekea nchini Kenya. Msemaji wa Wizara ya mali asili na utalii, Dorina Makaya amesema madai haya ”si ya kweli” kinachoendelea ni …

Read More »

WANAFUNZI UDOM KUFUNDISHWA USIMAMIZI KEMIKALI

OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeonesha nia ya kuanza kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa uhandisi wa uchenjuaji wa madini katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kauli hiyo ya kusudio imetolewa na Mkemia Mkuu, Dk Fidelice Mafumiko wakati wa kufunga mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa wanafunzi wa …

Read More »