Home / Habari za Kimataifa (page 221)

Habari za Kimataifa

App HIZI HUENDA ZINA NAMBA YAKO YA SIMU.

Siku hizi, kutokana na tabia ya watu kutumia programu tumishi kwa wingi kwenye simu zao, ni kawaida kwa nambari za simu za watu wenye kupatikana kwa urahisi mtandaoni. Uchunguzi unaonesha kwamba nambari za watu kama vile waziri mkuu wa zamani wa Uingereza David Cameron, kiongozi wa chama cha Leba Jeremy …

Read More »

CHANJO DHIDI YA UKIMWI KUFANYIWA MAJARIBIO AFRIKA KUSINI.

Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii. Wanasayansi wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo itafanikiwa, shirika la habari la AP linasema. Wakati wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN 702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao …

Read More »

MAANDAMANO YASITISHWA CUBA

Kundi maarufu linaloipinga serikali ya Cuba limesitisha maandamano yake ya kila wiki kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na tatu kufuatia kifo cha Fidel Castro ambaye wao wamekuwa wakimpinga kwa miaka yote. Kiongozi wa kundi hilo la wanawake maarufu kama Ladies in White, Berta Soler, amesema ametaka …

Read More »

FILLON AMSHINDA JUPPE KWENYE MCHUJO UFARANSA

Francois Fillon ndiye atakayekuwa mgombea urais wa chama cha wahafidhina nchini Ufaransa baada ya mpinzani wake Alain Juppe kukubali kushindwa. Baada ya kura nyingi kuhesabiwa, bw Fillon alikuwa anaongoza akiwa na karibu asilimia 67 ya kura zilizopigwa kwenye uchaguzi wa mchujo Jumapili. Bw Fillon ameahidi kuunda jamii yenye usawa na …

Read More »

MAMILIONI WASIOFAA KUPIGA KURA WALIPIGA,TRUMP ASEMA.

Rais Mteule Donald Trump amesema alishinda kwa wingi wa kura za kawaida “iwapo utaondoa kura za mamilioni ya watu ambao hawakufaa kupiga kura lakini walipiga”. Hata hivyo, hakutoa ushahidi wa kuthibitisha madai hayo yake. Mwanachama huyo wa Republican, alishinda uchaguzi kwa kura za wajumbe, ambazo ndizo huamua mshindi wa urais …

Read More »

SHAMBULIO LA KIKABILA LAUWA WATU 30 DRC CONGO

Wakuu katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wanasema, raia kama 30 wameuawa katika shambulio lililofanywa katika kijiji na wanamgambo wa kabila la Nande. Watu waliouawa katika jimbo la Kivu kaskazini, walikuwa wa kabila la Hutu – washindani wa miaka mingi na wa-Nande, mashariki mwa Congo. Watu waliuliwa kwa mapanga. Eneo …

Read More »

MFALME AKAMATWA KWA KUCHOCHOA GHASIA UGANDA.

Polisi nchini Uganda wanasema watu 50 wameuawa, katika mapambano baina ya askari wa usalama na kundi jipya lenye silaha, linalopigana kutaka kujitenga, magharibi mwa nchi. Polisi wamemkamata mfalme wa kabila la huko, Charles Wesley Mumbere, mfalme wa Rwenzururu, ambaye wanamshutumu kwa kuchochea fujo hizo. Amekanusha kuwa amehusika. Polisi pia wanasema …

Read More »

POLISI WAKABILIANA NA WAPIGANAJI WA MFALME UGANDA.

Takriban watu 14 wameuawa nchini Uganda ,katika makabiliano kati ya maafisa wa polisi na wapiganaji wanaohusishwa na mfalme mmoja wa kitamaduni nchini humo. Wapiganaji hao wanadaiwa kushambulia kituo kimoja cha polisi katika mji wa Magharibi wa Kasese ,ambao ndio nyumbani kwa mfamle wa Rwanzururu Charles Wesley Mumbere. Wapiganaji wanane pamoja …

Read More »

FIDEL CASTRO: MAGUFULI NA KENYATTA WATUMA RAMBIRAMBI

Rais Magufuli na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi waliotuma rambirambi zao Rais wa Tanzania John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi rais wa Cuba Raul Catsro kufuatia kifo cha rais mstaafu wa Cuba Fidel Castro. Katika salamu hizo magufuli amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za …

Read More »

WASICHANA MAHAKAMANI KWA KUPIGANA BUSU MOROCCO.

Wasichana wawili waliopatikana wakipigana busu katika paa la nyumba wamewasilishwa mahakamani katika mji wa Marrakesh nchini Morocco wakishtakiwa na tabia za wapenzi wa jinsia moja ,mmoja wa mawakili wao waliambia AFP. Wasichana hao wenye umri wa miaka 16 nad 17 mtawalia walishtakiwa kwa kushiriki tendo lililo kintume na maumbile yao. …

Read More »