Home / Habari Za Kitaifa / MNH kuhudumia wagonjwa wa dharura 300 kwa siku

MNH kuhudumia wagonjwa wa dharura 300 kwa siku

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imeboresha na kuongeza idadi ya wagonjwa wenye magonjwa ya dharura na ajali kutoka wagonjwa 100 hadi 150 na kufikia 200 hadi 300 kwa siku.

Aidha hospitali hiyo ipo katika mkakati wa kufanya upanuzi zaidi kwa ajili ya kuwepo huduma za dharura kwa watoto tu.

Ofisa Uhusiano wa MNH, John Steven alisema alipokuwa akizungumza na HabariLeo kuhusu maboresho hayo yaliyofanyika hospitalini hapo.

Alisema lengo la maboresho hayo ni kuwafikia wagonjwa wengi wanaofikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali au magonjwa ya dharura.

Alisisitiza kuwa maboresho hayo yanakwenda sambamba na ufungwaji wa vifaa vya kisasa vya kutoa huduma, ikiwa ni pamoja na kutumia madaktari bingwa ambao wamebobea katika eneo hilo.

Alisema Muhimbili ipo katika mstari wa mbele katika kufundisha hao wataalamu waliopo katika eneo hilo la ajali na magonjwa ya dharura.

Katika siku za karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la ajali pamoja na magonjwa ya dharura ambapo majeruhi na wagonjwa wanaopata magonjwa ya ghafla hufikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

Kutokana na ongezeko hilo, wataalamu wa tiba ya dharura nchini walipatiwa mafunzo ya vitendo jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha eneo hilo katika taasisi zote za afya.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *