Home / Habari za Kimataifa / Leseni ya mtoto kutoka kwa wazazi 3 yatolewa Uingereza

Leseni ya mtoto kutoka kwa wazazi 3 yatolewa Uingereza

Leseni ya mtoto anayezaliwa kutoka kwa wazazi watatu yaidhinishwa Uingereza

Madaktari mjini Newcastle nchini Uingereza wamepewa leseni ya kwanza nchini Uingereza kutengeza watoto kutoka kwa wanawake wawili na mwanamume mmoja, shirika la kuthibiti rutba limesema.

Mfumo huo mpya wa aina ya IVF utatumika kuwalinda watoto kutofariki kutokana na magonjwa yanayosambazwa kupitia jeni.

Kundi hilo katika kituo cha rutba za uzazi cha Newcastle kimesema kuwa ni habari njema kwa wagonjwa.

Na sasa kituo hicho sasa kinatarajia mtoto wa kwanza kuzaliwa 2018 ikiwa ndio mapema.

Mfumo huo unalenga kukabiliana na magonjwa ya jeni ambayo huwawacha watu kukosa nguvu za moyo wao kufanya kazi.

Baadhi ya watu wamepoteza watoto kadhaa kwa sababu ya ugonjwa huo.

Ugonjwa huo husambazwa kutoka kwa mama, kwa hivyo mbinu ya kutumia yai lililofadhiliwa, na yai la mama pamoja na mbegu za kiume za baba imeimarishwa.

Mtoto anayepatikana huwa na vinasaba vya jeni kutoka kwa mfadhili, lakini mfumo huo sasa ni wa haki na sasa unafuata maadili na uko tayari kufanyakazi kisayansi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *