Home / Habari za Kimataifa / Madereva walevi hulazimishwa kufanya kazi mochari Taiwan

Madereva walevi hulazimishwa kufanya kazi mochari Taiwan

Taiwan

Kenya , Tanzania, Uganda , Rwanda na hata Burundi utaona mabango makubwa yamewekwa kando ya barabara kuonya madereva kuto endesha magari wakiwa wamelewa .

Mabango hayo mbali na kukutishia kwamba unaweza kufariki kutokana na ajali, pia yanaonya kwamba ukipatikana utatozwa faini kubwa kama njia ya kukutia adabu kwa kosa la kuendesha gari ukiwa mlevi.

Lakini nchini Taiwan mambo ni tofauti kabisa.

Dereva yeyote anayepatikana na kosa la kuendesha gari akiwa mlevi , anakamatwa na kupelekwa kwenda kufanya kazi katika chumba cha kuhifahdi maiti.

Mkuu wa mashtaka katika jimbo la Taitung huko Taiwan, ameiambia BBC kwamba madereva wanaopatikana na kosa la kuendesha gari wakiwa wamelewa wanapewa kazi maalum ya kusafisha meza za kuwa pasulia maiti. Na pia wanatakina kuosha na kusafisha kabisa friji za kuwekea maiti.

Sababu kubwa hasa ya kufanya hivyo ni kuwapa madereva hao fursa ya kuona maiti hasa zile zitokanazo na ajali za barabarani

Sababu kubwa hasa ya kufanya hivyo ni kuwapa madereva hao fursa ya kuona maiti hasa zile zitokanazo na ajali za barabarani jinsi zilivyo pondeka pondeka zinapoletwa na hata kutolewa kutoka hizo mochari.

Wakuu wa mashtaka wanatarajia kwamba pengine fursa ya kuona maiti hizo zitawafunza jinsi gani maisha ni muhimu na ni sharti ya heshimiwe kwa dereva kuwa waangalifu barabarani na kuepuka na tabia ya kuendesha gari ukiwa umelewa.

Badala ya watu kupinga adhabu hiyo, sasa mitandao ya kijamii imejaa kauli za watu wakisema badala ya kupanguza tu meza za upasuaji maiti pamoja na friji za kuwekea maiti hizo.

Ukipatikana na kosa la kuendesha gari ukiwa umelewa bora upewe adhabu ya kuosha maiti , tena maiti za watu waliofariki kutokana na ajali za barabarani.

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *