Home / Habari Za Kitaifa / Magufuli- Nitafuatilia mwenyewe

Magufuli- Nitafuatilia mwenyewe

“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.”

Rais Joh Magufuli amesema hayo wakati akimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi wilayani humo.

Akaongeza, “Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi, wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Rais Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam alitoa agizo hilo jana aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.

Baada ya kusimamisha msafara wake, aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitokeza alisema wafugaji wa jamii za Wamang’ati wamekuwa wakiingiza mifugo katika mashamba ya mazao yao na wanapojaribu kuwakatza, wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.

Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe, Rais Magufuli alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji.

Kadhalika, alimtaka kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo wao katika mashamba ya wakulima.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *