Home / Habari za Kimataifa / Benki ya dunia yatangaza msaada wa dola milioni 57 kwa nchi za Afrika

Benki ya dunia yatangaza msaada wa dola milioni 57 kwa nchi za Afrika

Sehemu kubwa ya msaada huo utatumiwa katika kutoa dhamana kwa mikopo isiyo na riba kwa baadhi ya mataifa maskini zaidi duniani .

Benki ya dunia imetangaza msaada wa miaka mitatu kwa mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la sahara wenye thamani ya dola bilioni 57.

Sehemu kubwa ya msaada huo utatumiwa katika kutoa dhamana kwa mikopo isiyo na riba kwa baadhi ya mataifa maskini zaidi duniani .

Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim anasema udhamini huo wa kifedha utayasaidia mataifa ya Afrika kuwa na ukuaji wa kiuchumi , kubuni nafasi za ukuaji huo pamoja na kuyalinda dhidi ya hasara na mizozo ya kiuchumi .

Kiwango cha pesa zenye thamani ya dola bilioni 45 kitatolewa kwa mataifa hayo kupitia Jumuiya ya kimataifa ya Maendeleo, ikiwa ni kitengo cha Benki ya dunia kinachohusika zaidi na mataifa maskini zaidi duniani .

Msaada huo wa fedha utasaidia kuboresha miradi 400 inayoendelea katika mataifa yaliyoko chini ya jangwa la sahara, kuanzia ile inayohusika na maendeleo ya miundo mbinu , elimu, utoaji wa huduma ya maji safi na huduma za afya za msingi.

Lengo ni kubuni hali itakayoweza kuinua uchumi na wachambuzi wanasema msaada huu kutoka benki ya dunia, unaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuimarika kwa mchakato wa kufufua uchumi wa mataifa hayo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *