Home / Habari Za Kitaifa / Dola mil 51 kujenga barabara kuunganisha Dar

Dola mil 51 kujenga barabara kuunganisha Dar

TANZANIA imetia saini na Serikali ya Kuwait kuhusu mkopo wa Dola za Marekani milioni 51 (Sh bilioni 109.69) kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua- Chaya yenye urefu wa kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami kuunganisha Dar es Salaam na mikoa ya Mashariki na Magharibi nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alisema ujenzi wa barabara hiyo ni muhimu kutokana na kuwa kiunganishi kati ya maeneo ya Mashariki mwa Tanzania, mikoa ya Magharibi na nchi jirani za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Jiji la Dar es Salaam ikipitia katika mikoa mitatu hadi Kigoma.

Barabara ya Nyahua-Chaya ni sehemu ya barabara kati ya Itigi na Tabora. Alisema lengo la mradi huo ni kuongeza ufanisi wa usafiri kati ya Bandari ya Dar es Salaam na Kigoma na nchi jirani, na kupunguza gharama za usafirishaji kati ya maeneo hayo.

Alisema mkopo uliosainiwa jana una vipengele vitatu ambavyo ni kazi ya ujenzi wa barabara, madaraja na mifumo ya kupitisha maji. Kipengele kingine ni fedha za malipo ya ushauri wa mradi na fedha za kufanyia upembuzi yakinifu.

“Makubaliano haya yanaonesha utayari wa Serikali ya Kuwait kuendelea kuisaidia Tanzania ambayo wamekuwa na uhusiano mzuri kwa miongo kadhaa sasa,” alisema Dk Mpango.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *