Home / Habari za Kimataifa / Bemba ahukumiwa mwaka mmoja jela na ICC kwa utoaji hongo

Bemba ahukumiwa mwaka mmoja jela na ICC kwa utoaji hongo

Bemba tayari ametumikia kifungo miaka kumi na minane ya kifungo chake gerezani kwa uhalifu wa kivita

Makamu wa zamani wa rais nchini DRC ean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na mahakama ya kimataifa ya uhalivu ICC kwa kutoa hongo kwa mashahidi kuongezea miaka 18 ambayo tayarii amekwishatumikia jela kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa Bwana Bemba ameamrishwa kulipa faini ya ya dola $323,500; kwa kuwahonga mashahidi katika kesi yake ya uhalifu wa kivita.

Katika kesi ya kwanza kuwahi kusikilizwa kuhusu ufisadi mahakama hiyo ilimsikiliza Bwana Bemba na washirika wake wanne waliopewa hongo na kuweza kuwafanya mashahidi muhimu wapatao wanne wabadilishe ushahidi wao katika kesi ya uhalifu wa kivita dhidi yake mapema mwaka huu.

Tayari ametumikia miaka kumi na minane ya kifungo chake gerezani kwa uhalifu huo.

Bwana Bemba, wakili wake, meneja wa kesi yake, mwanasiasa mwingine na shahidi wa upande wa utetezi wote wanakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela , faini ama adhabo zote kwa pamoja.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *