Home / Habari za Kimataifa / Hosni Mubarak aachiliwa huru Misri

Hosni Mubarak aachiliwa huru Misri

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubaraka ameachiliwa huru baada ya kuhudumia kifungo cha miaka kadhaa

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak ameripotiwa kuachiliwa huru baada ya kuhudumia miaka jela kufuatia maandamano yaliomng’atuwa mamlakani 2011.

Bwana Mubarak alikuwa akizuiliwa katika hospitali ya kijeshi mjini Cairo, lakini wakili wake aliiambia BBC kwamba sasa ameruhusiwa kurudi nyumbani kwake mjini humo.

Aliagizwa kuachiliwa huru mapema mwezi huu baada ya mahakama ya rufaa kumuondolea makosa ya kuwaua waandamanaji wakati wa maandamano dhidi yake 2011.

Bwana Mubarak mwenye umri wa miaka 88 alichukua mamlaka 1981 baada ya mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Anwar Sadat.

Amekuwa akizuiliwa katika hospitali ya kijeshi ya Maadi tangu 2013 baada ya kuhamishwa katika eneo hilo kwa dhamana kutoka jela ya Torah.

Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia 2012 ya mauaji ya waandamanaji waliouawa katika mikono ya vikosi vya usalama mnamo mwezi Februari 2011.

Kesi nyengine ilianzishwa na jaji akaamuru kwamba Mubaraka anaweza kutolewa mwezi Mei 2015.

Hatahivyo serikali ya rais Abdul Fattah al-Sisi iliripotiwa kwamba haipo tayari kumuachilia huru kutokana na upinzani ambao huenda ungejitokeza miongoni mwa raia iwapo ataachiliwa.

Bwana Sisi alihudumu kama mkuu wa kitengo cha ujasusi cha rais Mubarak katika jeshi na aliongoza jeshi kumuondoa madarakani mrithi wa Mubarak, Mohammed Morsi 2013.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *