Home / Habari za Kimataifa / Marekani kuanzisha uchunguzi kwa mashambulizi ya Mosul,Iraq

Marekani kuanzisha uchunguzi kwa mashambulizi ya Mosul,Iraq

Mapigano yanayoendelea Mosul yamesababisha mamia ya watu kufariki ukiachilia mbali kupoteza makazi yao

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa inaanzisha uchunguzi juu ya tuhuma za ndege za nchi hiyo kushambulia wananchi wasiokuwa na hatia katika mji wa Mosul nchini Iraq mapema mwezi huu.

Katika kulishughulikia jambo hilo, zaidi ya mikanda ya video mia saba itachunguzwa.

Msemaji wa jeshi la Marekani kanali J T Thomas amesema kuwa jeshi la nchi hiyo lilifanya mashambulizi karibu na eneo hilo lakini hawakulifikia.

Ameongeza kuwa hakuna mabadiliko katika kupambana na vikosi vya IS na hawatarudi nyuma.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *