Home / Habari Za Kitaifa / Rugimbana apewa siku 3 ajibu ripoti ya tume

Rugimbana apewa siku 3 ajibu ripoti ya tume

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma limetoa siku tatu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kutoa majibu ya ripoti ya tume ya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha dhidi ya Meya wa manispaa hiyo, Jafari Mwanyemba.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi alikataa hoja za madiwani hao za kutaka Meya anyang’anywe gari, kutotumia ofisi kwa madai kuwa tume haijatoa taarifa, akisema kuwa kufanya hivyo kutasimamisha shughuli mbalimbali za maendeleo kwani kuna nyaraka zinazohitaji kusainiwa.

Hayo yalibainika katika kikao maalumu cha dharura kilichoitishwa na baraza hilo ii kujua hatma ya Meya Mwanyemba anayekabiliwa na ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh milioni 30.

Kunambi alisema suala la usafiri wa meya anatakiwa kuwezeshwa kwa siku mbili za juma.

“Tusivuruge, tusifute kanuni kwa mikataba, faili zisiposainiwa yale yaliyoamriwa kufanyika yatasimama lazima tuache yaendelee wakati tukisubiri taratibu nyingine,” alieleza.

Alisema amekubaliana na maamuzi ya baraza hilo na kuahidi kumuandikia barua Mkuu wa Mkoa ili awasilishe ripoti ndani ya siku tatu walizoomba.

Alisema kanuni zinazoendesha manispaa ya Dodoma ndio msingi wa shughuli za kila siku, ambapo ilitakiwa ndani ya siku tatu meya aliyeandikiwa barua ajibu ndani ya siku tano, jambo alilolitekeleza kwa kukabidhi majibu yake kwa Mkurugenzi.

Alisema baadaye Mkuu wa Mkoa aliunda tume ya uchunguzi wa sakata hilo ambalo madiwani wanalalamikia kuchelewa kwa majibu ya uamuzi huo.

Diwani wa Kata ya Mbabala, Paskazia Mayala alisema Halmashauri si ya mtu inasimamia kanuni na taratibu.

“Sasa kwenye sakata hili hata wataalamu wameingia tunaomba wakae pembeni, Mwanyemba tulimchagua wenyewe na tutamuondoa wenyewe. Leo siku ya 12 hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na tume ya uchunguzi iiyoundwa na Mkuu wa Mkoa,” alieleza na kudai kuwa wako tayari kuona baraza la madiwani likivunjwa kwani wanafanya kazi kwa niaba ya wananchi na hawana sababu ya kumuonea mtu aibu.

Diwani wa Chahwa, Sospeter Mazengo alisema tume hiyo isilazimishe madiwani kuvunja kanuni kwani siku 12 zimepita bila tume hiyo kutoa taarifa, huku Diwani wa Matumbulu, Emmanuel Chibago akieleza kuwa kila kitu kina utaratibu wake na taratibu zote zimefanyika na suala hilo kufika kwa mkuu wa mkoa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *