Home / Habari za Kimataifa / Makamu wa rais Afrika Kusini akosoa kufutwa kazi waziri wa fedha

Makamu wa rais Afrika Kusini akosoa kufutwa kazi waziri wa fedha

Bwana Ramaphosa (kushoto) alisema kuwa hatajiuzulu

Makamu wa rais nchini Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameitaja hatua ya kufutwa kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan kuwa isiyokubalika.

Kufutwa kazi kwa Gordhana kumesababisha masoko ya hisa kushuka kwa asilimia 5.

Bwana Gordhan alionekana kama mpinzani mkubwa wa ufisadi kwenye uongozi ambao umekosolewa vikali.

Aikuwa mmoja wa mawaziri waliofutwa kazi wakati Rais Jacob Zuma, alilifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.

Bwana Ramaphosa alikiambia kituoa cha habari cha SABC kuwa hatajiuzulu kufuatia kufutwa kwa mawaziri hao bali ataendelea kuwatumikia watu.

Mr Gordhan remained defiant in the wake of his sacking

Pravin Gordhan alitajwa na wengi kama mtu mwenye tajriba ya kusimamia uchumi.

Alikuwa akizuia matumizi makubwa ya serikali na kukataa wito wa rais wa kutaka matumizi ya serikali kuongezwa.

Huu ndiyo duru ya pili bwana Gordhan anahudumu kama waziri wa fedha baada ya kuhudumu kwanza kati ya mwaka 2009 na 2014.

Aliteuliwa mwaka 2015 kuchukua mahala pa David van Rooyen. Uteuzi wa bwana Van Rooyen ulikumbwa na utata na alihudumu kama waziri wa fedha kwa muda wa wiki moja.

Cyril Ramaphosa, Jacob Zuma na Pravin Gordhan wakati wa siku ya kusomwa bajeti mwezi uliopita

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *