Home / Michezo / Waziri mkuu wa Canada kupigana ndondi na mcheza filamu

Waziri mkuu wa Canada kupigana ndondi na mcheza filamu

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau akiwa kwenye Mazoezi mwaka 2012

Katika historia ya masumbwi ni majina machache yaliyo maarufu

Muhammad Ali na Joe Frazier. Evander Holyfield na Mike Tyson. Sugar Ray Leonard na Tommy Hearns.

Na sasa pambano linalokuja ni kati ya Matthew Perry na Justin Trudeau.

Mcheza filamu Matthew Perry na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, wamesema kuwa huenda wakapimana nguvu baada ya bwana Tradeau kutaka pigano lilofanyika shuleni miaka 35 iliyopita kurudiwa.

Ujumbe ambao Trudeau aliandika kwenye mtandao wa Twitter tarehe mosi mwezi Aprili, ulikuja baada ya bwana Petty kukiri kuwa wakati mmoja alimtandika bwana Trudeau.

Ujumbe kutoka kwa Justin Trudeau

Perry aliakiambia kituo kimoja cha runinga cha Marekani kuwa wote walikuwa shule moja ya msingi huko Ottawa, wakati yeye na rafiki wake waliamua kumpiga kijana huyo mdogo.

“Nafikiri alikuwa mtoto peke yake ambaye nilikuwa na uwezo kumpiga,” Perry alisema.

Mambo hata hivyo yamebadilika miaka iliyopita. Perry amekuwa mmoja wa watu maarufu katika sekta ya filamu duniani.

Naye bawana Trudeau ambaye anataja ndondi kama mchezo anaoupenda amefuata nyayo za babake na kuwa waziri mkuu wa Canada.

Ujumbe kutoka kwa Matthew Perry

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *