Home / Michezo / Serengeti Boys yaigomea Ghana, yachomoa mbili dakika za majeruhi

Serengeti Boys yaigomea Ghana, yachomoa mbili dakika za majeruhi

Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys imetoka nyuma mara mbili na kuilazimisha sare ya mabao 2-2  timu ya Taifa ya vijana wa umri huo ya Ghana maarufu kama Black Starlets katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya kujipima nguvu.

Mechi hii imepigwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa na kushuhudia wenyeji Serengeti Boys wakifanikiwa kulinda rekodi yao ya kutofungwa nyumbani.

Mabao ya Serengeti yalifungwa  kipindi cha dakika kumi za nyongeza kupitia kwa Assad Juma aliyekwamisha mkwaju wa penati dakika ya 95 na Mukhsin Malima aliyefunga dakika ya mwisho ya nyongeza.

Ghana walionekana kutawala kipindi cha kwanza walipata bao lao kwanza kupitia Sulley Ibrahim aliyeachia mkwaju mkali nje ya eneo la kumi nane na kumzidi kipa wa Serengeti Ramadhan Kabwili.

Walikuwa ni Ghana tena waliopata bao la pili baada ya kipindi cha pili kuanza. Kiungo mkabaji wa Serengeti Boys, Ally Ng’anzi alifanya makosa ya kumchezea rafu Mensah ndipo mwamuzi alipoamuru pigo huru nje kidogo ya eneneo la hatari la Tanzania.

Mkwaju wa Mensah ulikwenda moja kwa moja katika paa la lango la Serengeti Boys huku kipa Ramadhan akichupa bila mafanikio.

Baada ya mchezo huu, Serengeti Boys wanatarajiwa kuelekea Morocco kwa ajili ya kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na maandalizi ya mwisho ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *