Home / Habari za Kimataifa / Chanjo kubwa dhidi ya homa ya uti wa mgongo yaanza kutolewa Nigeria

Chanjo kubwa dhidi ya homa ya uti wa mgongo yaanza kutolewa Nigeria

Chonjo kubwa dhidi ya homa ya uti wa mgongo yaanza kutolewa Nigeria

Watoa huduma za afya nchini Nigeria wameanza shughuli ya kutoa chanjo dhdi ya homa ya uti wa mgongo.

Zaidi ya watu 300 wamefariki kutokana na ugonjwa huo tangu mwaka uliopita.

Watoa huduma za afya wanalenga zaidi jimbo la kaskazin magharibi la Zamfara, ambalo ndilo kitovu cha mlipuo wa ugonjwa huo.

Idara ya kukabiliana an magonjwa nchini Nigeria inasema kuwa chanjo 500,000 zilitatolewa.

Maafisa wa afya wanasema kuwa karibu watu 3000 wanashukiwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Hadi sasa watu walioathirika zaidi ni watoto walio kati ya umri wa miaka 5 na 14.

Afisa mmoja aliiambia BBC kuwa jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zimetatizwa na uhaba wa dawa za kutoa chanjo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *