Home / Habari Za Kitaifa / Wazazi wanaotelekeza watoto kudhibitiwa

Wazazi wanaotelekeza watoto kudhibitiwa

IDARA ya Ustawi wa Jamii imeagizwa kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wazazi ambao hawatekelezi majukumu yao ya kuwalea watoto, hivyo kuwafanya kuzagaa mitaani.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyasema hayo bungeni mjini hapa alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF) ambaye pamoja na mambo mengine alitaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali katika kupunguza tatizo la watoto wa mitaani.

Waziri Ummy alisema ni kweli kwamba kumekuwa na ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hasa katika miji mikubwa nchini.

Alisema kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika katika majiji ya Dar es Salaam na Mwanza mwaka 2012 zilionesha kuwa Jiji la Dar es Salaam lilikuwa na watoto 5,600 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiongozwa na Dar es Salaam yenye asilimia 28.

Mikoa mingine na asilimia zake kwenye mabano ni Dodoma (9), Mwanza (7), Morogoro (7), Tanga (6), Lindi (6), Iringa (5), Pwani (5), Kilimanjaro (5) na Arusha (4).

“Serikali inalo jukumu la msingi kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watoto. Ili kutekeleza wajibu huu serikali kwa kushirikiana na wadau inatekeleza mikakati mbalimbali, Mojawapo ya mikakati hii ni kuwezesha jamii kuwa na mipango shirikishi jamii ya kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, wakiwemo watoto wa mitaani, Hadi sasa mpango huu unatekelezwa katika halmashauri 111.

Aidha Wizara kwa kushirikiana na Tamisemi imeanzisha mpango wa kuimarisha ulinzi na usalama kwa watoto ambapo halmashauri 51 zimewezeshwa kuunda timu za ulinzi wa watoto. Serikali itaendelea kueneza mpango huu katika halmashauri nyingine,” alisema.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *