Home / Habari Za Kitaifa / 5,000 kupata huduma za macho Kigoma

5,000 kupata huduma za macho Kigoma

UHABA mkubwa wa madaktari wa macho na gharama kubwa za matibabu imeelezwa kuwa ni kikwazo kikubwa kwa wananchi wenye kipato duni kupata huduma za matibabu ya macho na hivyo kusababisha kuwapo kwa watu wengi wenye upofu.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Bilali Muslim Barani Afrika, Mohsin Abdallah amesema hayo katika uzinduzi wa kambi ya siku nne ya matibabu ya macho iliyoanza Aprili 14 mwaka huu inayofanyika kijiji cha Ilagala wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo wananchi zaidi ya 5,000 wanatarajia kupata huduma hiyo.

Abdallah alisema kuwa kwa kiasi kikubwa huduma za matibabu ya macho zimekuwa zikipatikana katika hospitali za mikoa na baadhi ya hopsitali za wilaya mkoani humo hivyo sehemu kubwa ya vituo vya afya na zahanati havina huduma hizo na hivyo kufanya watu wengi wenye kipato duni kutoka vijijini kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Taasisi ya Bilali Muslim Mission imekuwa ikifanya huduma za kambi ya macho maeneo mbalimbali ya vijijini kwenye mikoa mbalimbali nchini ili kuwafikia wananchi hao ambapo huduma za upimaji, operesheni na utoaji wa miwani na dawa hufanyika.

Katika kambi hiyo ya siku nne Abdalla alisema kuwa kundi la Madaktari 25 na watoa huduma wa kujitolea kutoka mikoa mbalimbali nchini watatoa huduma katika kambi hiyo. Kwa upande wake Mratibu wa kambi za matibabu za macho za Taasisi ya Bilali Muslim, Aini Sharifu alisema kuwa jumla ya wananchi 50,000 kutoka mikoa mbalimbali wameweza kupatiwa matibabu ya macho na taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka 10 ambayo matibabu yamekuwa yakifanyika kwenye kambi za macho zinazofanywa na Taasisi hiyo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

wakulima tanzania

Wakulima Tanzania watafuta masuluhisho kwa changamoto zao

Wakulima nchini Tanzania wameonya kuwa huenda nchi hiyo ikaingia kwenye baa la njaa kutokana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *