Home / Habari za Kimataifa / Mwigulu aelekeza ulipaji stahiki Polisi

Mwigulu aelekeza ulipaji stahiki Polisi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ameielekeza Wizara yake na Jeshi la Polisi Makao Makuu kuhakikisha wanatoa stahiki za askari wanaopata matatizo wanapokuwa wakitekeleza shughuli za jeshi hilo.

Mwigulu alitoa maelekezo hayo jana wakati akiongoza mamia ya askari na wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuaga miili ya askari nane waliouawa na majambazi eneo la Mkengeni, kata ya Mjawa, Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

Kauli hiyo ya Mwigulu imekuja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu kumtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro na Lindi ambapo askari nane waliouawa wametoka katika mikoa hiyo kuhakikisha wanakamilisha taratibu ili ndugu kupata haki zao kwa wakati kwa kuwa wana watu ambao wanawategemea.

Mwigulu alisema vitu vinavyotokea ni vya wazi hivyo vishughulikiwe kwa haraka na kuacha kufuata taratibu ambazo hazina ulazima badala yake washughulikie kwa utaratibu wa kuangalia mazingira.

Alisema askari wanaopata matatizo wanakuwa mstari wa mbele katika matukio lakini wanaokaa nyuma wanakwamisha kwa kuwa hawajui shida wanayoipata askari hao. Aidha Mwigulu alisema anataka kuona mafaili yote yanayowahusu askari hao waliouwawa kushughulikiwa kwa haraka ili kuwasaidia wafiwa ambao wengi walikuwa wakiwategemea.

Aidha alisema ili kuhakikisha stahiki zinatakiwa zinapatikana kwa wakati wataangalia upya sheria zinazosimamia upatikanaji wa stahiki hizo ili kuwezesha kupatikana bila kufuata utaratibu mrefu.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *