Home / Habari za Kimataifa / Mhubiri kutoka DRC Joseph Mutombo apewa hifadhi Afrika Kusini

Mhubiri kutoka DRC Joseph Mutombo apewa hifadhi Afrika Kusini

Mhubiri kutoka Kongo Paul Joseph Mutombo anampinga Rais Joseph Kabila na ameukosoa utawala wake sana.

Mhubiri aliyewahi kuwania urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Mutombo amepewa hifadhi ya kisiasa nchini Afrika Kusini baada ya miaka kadhaa ya vuta nikuvute kuhusu hatma yake, taarifa zinasema.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ilitaka arejeshwe nchini mwake huku ikimshutumu kwa jaribio la mapinduzi ya serikali miaka mitatu iliyopita, wakati wafuasi wake walishambulia maeneo muhimu na kudhibiti kwa muda mfupi makao makuu ya shirika la kitaifa la utangazaji.

Mutombo alitorokea nchini Afrika Kusini lakini alikamatwa baada ya Interpol kutoa idhini.

Msemaji wake alisema kuwa atakuwa huru kuendesha kampeni ya kumtoa rais Joseph Kabila mamlakani akiwa ugenini.

Kabila amekataa uchaguzi mpya ufanywe licha ya wakati wake mamlakani kukamilika Desemba mwaka uliopita.

Maafisa wa Afrika Kusini hawajasema lolote kuhusu suala hili.

Hapo awali, walikuwa wamekataa kumpa mhubiri huyo hifadhi ya kisiasa.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo inataka Mukungubila, ambaye anajitambulisha kama “Mjumbe wa mwisho kwa binadamu kutoka kwa Mungu” atoe majibu kuhusiana na vurugu ambazo zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

Serikali ya DRC inamlaumu kwa kuchochea mfululizo wa mashambulizi mnamo Desemba mwaka wa 2013 katika uwanja wa ndege, makao makuu ya jeshi na katika mji mkuu wa Lubumbashi.

Alitorokea Afrika Kusini ambako alikamatwa mwezi Mei, mwaka wa 2014 katika nyumba yake, huko Johannesburg kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.

Wakati huo, wakili wake alisema alikuwa anashtakiwa kwa makosa ya mauaji, mashambulio ya kukusudia, uchochezi, uharibifu wa mali na kuzuiliwa kwa watu kwa njia kiharamu.

Mamlaka ya Afrika Kusini hatimaye walitupilia mbali kesi kwa madai ya ukosefu wa ushahidi.

Mutombo, ambaye anakanusha madai dhidi yake, anampinga Rais Joseph Kabila na ameukosoa utawala wake sana.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *