Home / Habari za Kimataifa / Mzaliwa wa Kenya Lucy Gichuhi athibitishwa kuwa seneta Australia

Mzaliwa wa Kenya Lucy Gichuhi athibitishwa kuwa seneta Australia

Seneta Gichuhi ambaye ni mzaliwa wa Kenya

Mahakama kuu nchini Australia imefutilia mbali juhudi za chama cha Labor kupinga kuidhinishwa kwa mwanasiasa mzaliwa wa Kenya Lucy Gichuhi kuwa seneta nchini humo.

Chama hicho kilikuwa kimeumbua maswali kuhusu uraia wa Bi Gichuhi ambaye ni wa chama cha Family First.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABC la Australia, Mahakama Kuu nchini humo imetangaza kwamba Bi Gichuhi yuko huru kumrithi mwenzake kutoka chama cha Family First -FF, Bw Bob Day, ambaye awali alishinda kwenye uchaguzi, lakini akalazimishwa kuachia kiti hicho.

Kaimu mwanasheria mkuu katika chama cha Labor Katy Gallagher alisema kuwa kulikuwa na maswali tata kuhusu uhalali wake ambayo yalitakiwa kujibiwa.

Lakini wajaji wote wa jopo la Mahakama ya Juu waliunga mkono kutupilia mbali ombi la mawakili wa Labor Anne McEwen, ambaye alitaka ijulikanie wazi iwapo Seneta Gichuhi angali raia wa Kenya.

Wakili Gichuhi ambaye ni mzaliwa wa Kenya alihamia Australia mwaka wa 1999 na alisema alikuwa raia wa Australia mwaka wa 2001 na hajawahi kuwa na na uraia wa nchi mbili.

Katiba ya Australia inamkataza mtu yeyote ambaye ni raia wa nchi mbili kuingia bungeni.

Haijulikani bayana iwapo Bi Gichuhi alipaswa kutoa ushahidi wa kuonyesha kuwa alikana uraia wa Kenya kabla ya kupigania kuwa bungeni.

Seneta Gichuhi alitoa ujumbe mfupi kwa wanahabari baada ya maamuzi ya mahakama, lakini hakuchukua maswali.

ABC imemnukuu akisema: “Haya hayanihusu mimi kama Lucy Gichuhi. Ni kuhusu uadilifu wa tasisi zilizo nchini”.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *