Home / Habari za Kimataifa / OPCW: Gesi ya Sarin ilitumika kwenye mashambulizi Syria

OPCW: Gesi ya Sarin ilitumika kwenye mashambulizi Syria

Walioathirika wengi wao ni Watoto

Majibu ya uchunguzi nchini Syria yanaonyesha kuwa Gesi ya Sarin au kemikali ya kufanana na hiyo ilitumika kwenye silaha za kemikali kutekeleza mashambulizi nchini Syria mapema mwezi huu, Shirika la kuzuia matumizi ya silaha za kemikali (OPCW) limeeleza.

Sampuli kutoka kwa waathirika 10 zimefanyiwa tathimini katika maabara nne, mkuu wa Shirika hilo Ahmet Uzumcu ameeleza.

Shambulio katika mji unaodhibitiwa na waasi, Khan Sheikhoun liligharimu maisha ya watu takribani 87.

Majeshi ya Syria yalikana kutumia gesi ya kemikali.

Mshirika wa Syria, Urusi imesema shambulio la anga lilipiga ghala lenye silaha za kemikali la waasi , lakini utetezi huo ulikataliwa.

Picha za Video zilionyesha raia wengi wao watoto wakikohoa na kutokwa povu mdomoni

Shirika la OPCW linaendelea kufanya mahojiano na kukusanya sampuli.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *