Home / Habari Za Kitaifa / Mtoto wa ugonjwa wa ngozi Rukwa aanza kutibiwa

Mtoto wa ugonjwa wa ngozi Rukwa aanza kutibiwa

MTOTO Peter Kazumba (13) na mdogo wake anayemfuata mwenye umri wa miaka 10 wamelazwa katika Hospitali Teule ya Wilaya (DDH) iliyopo katika Mji wa Namanyere katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kwa matibabu wakiwa chini ya uangalizi wa mtaalamu wa magonjwa ya ngozi.

Kulazwa kwa wana ndugu hao katika hospitali hiyo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Steven alilolitoa jana alipoitembelea familia ya mtoto huyo inayoishi katika Kitongoji cha Nkata kilichopo katika Kata ya Kate wilayani Nkasi.

Zelothe alimwagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk Emmanuel Mtika, ahakikishe mtoto Peter anayesumbuliwa na ugonjwa sugu wa ngozi, anapelekwa haraka katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa iliyopo Sumbawanga Mjini kwa matibabu.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Mtika alisema kuwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitolitoa juzi limetekelezwa ambapo alimwagiza mtaalamu wa ugonjwa wa ngozi kufika katika kitongoji hicho na kuiona familia hiyo.

Alisema baada ya mtaalamu huyo kukutana na familia hiyo licha ya mtoto Peter kuumizwa na ugonjwa huo wa ngozi pia alibaini kuwa hata mdogo wake anayemfuata mwenye umri wa miaka 10 naye ameumizwa na ugonjwa huo.

“Kwa sasa tunasubiri matokeo ya uchunguzi wa kimaabara ambao utabaini ugonjwa huo unaowasumbua watoto hao wawili,” alieleza. Kwa mujibu wa Dk Mtika mtaalamu huyo wa magonjwa ya ngozi akiwa katika familia hiyo amebaini kuwa baba na mama wa familia hiyo pamoja na watoto wao wengine wamepata maambukizi ya ugonjwa wa ngozi ambao ni mchanganyiko wa fangasi na bakteria ambapo watatibiwa wakiwa nyumbani hapo.

Mtoto Peter ambaye hasomi na hajawahi kuingia darasani anaishi na wazazi wake katika kitongoji cha Nkata kilichopo katika Kata ya Kate wilayani Nkasi, akiwa anasumbuliwa na ugonjwa sugu wa ngozi kwa zaidi ya miaka mitano bila kupona.

Ugonjwa huo umemfanya aharibike na kutoa harufu kali, huku akiwa na jeraha kubwa la moto katika goti lake la mguu wa kushoto na anaonekana mzee kuliko umri wake.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *