Home / Habari Za Kitaifa / Alazimishwa kula kinyesi kwa kumtukana mama yake

Alazimishwa kula kinyesi kwa kumtukana mama yake

WANAWAKE wa kijiji cha Kisungamile kilichopo katika Kata ya Matai wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wamemwadhibu Vitus Nyami (26) kwa kumtembeza nusu uchi na kulazimisha kula kinyesi cha ng’ombe kwa kosa la kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni.

Aidha wanawake hao walitumia mfuko wa ‘salphate’ kufunika sehemu za siri za kijana huyo kisha wakaanza kumtembeza mitaani kijiji humo huku wakiimba nyimbo za kabila la Kifipa wakilaani tabia ya kijana huyo ya kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni kila kukicha .

Walidai kukasirishwa na tabia ya kijana huyo wa kiume kumtukana mzazi wake wa kike matusi ya nguoni, hivyo walilazimika kumfunga kamba na kumtembeza mitaani kijijini humo akiwa nusu uchi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kisungamile, Didas Musa alikiri kutokea kwa mkasa huo juzi ambapo mtuhumiwa huyo alitembezwa mitaani kwa saa sita kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

Akifafanua alisema kuwa licha ya adhabu hiyo ya kutembezwa nusu uchi mitaani na kucharazwa viboko 15, pia ameamriwa kulipa mbuzi mmoja, unga wa sembe debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.

“Adhabu hii kwa kijana hutolewa na akina mama ambapo mimi kama kiongozi kazi yangu ni kuibariki tu,” alisisitiza . Mkazi wa kijiji hicho, Obedi Mwanakatwe alisema kijana huyo amekuwa akimtukana mama yake mara kwa mara , tabia ambayo imekuwa ikiwachukiza akinamama kijijini humo ambapo waliandamana na kumkamata kijana huyo .

“Baada ya akinamama hao wenye hasiri kumkamata kijana huyo walimpeleka kwenye shimo lililojaa kinyesi cha ng’ombe kisha wakampaka kinyesi hicho mwili mzima wakiwa wamechanganya na unga wakisaidiwa na wanaume, walimtembeza uchi kijana huyo mitaani kijijini humo,” alieleza.

Stela Tenganamba alisema baada ya kumtembeza kwa muda mrefu walimua kumlisha kinyesi cha ng’ombe na kumpaka mwili mzima sambamba na kumroweka kwenye matope.

Adhabu hiyo iliwekwa enzi za mababu zao , ambapo mtu yeyote anayetukana matusi hadharani huchukuliwa hatua hiyo sambamba na kulipishwa ng’ombe mmoja, mbuzi, unga debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.

Akifafanua alisema kuwa baada ya kutembezwa mitaani akiwa uchi hupelekwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambaye hutoa adhabu kulingana na akinamama watavyoona inafaa

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *