Home / Habari za Kimataifa / Watu 24 wafariki ajalini Mtito Andei, Kenya

Watu 24 wafariki ajalini Mtito Andei, Kenya

Basi hilo lilikuwa linaelekea Mombasa ajali ilipotokea

Watu 24 wamefariki na wengine kadha kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa manane katika barabara kuu ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.

Ajali hiyo iliyohusisha basi la kubeba abiria na lori la kusafirisha mafuta ghafi ya kupikia ilitokea katika eneo la Kambu, karibu na Mtito Andei.

Mkuu wa polisi wa eneo la Kibwezi Leonard Kimaiyo ameambia BBC kuwa watu 23 walifariki papo hapo na mwingine mmoja akafariki akitibiwa hospitalini.

Watu 20 walipata majeraha na kupelekwa katika hospitali za miji ya Kibwezi na Makindu.

Bw Kimaiyo amesema walionusurika waliambia maafisa wa polisi dereva wa basi alikuwa akijaribu kupita gari jingine basi lilipogongana na lori hilo.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Uchukuzi Kenya, watu 3,000 hufariki kila mwaka kutokana an ajali za barabarani.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *