Home / Habari za Kimataifa / Wanasayansi wagundua viwavi wanaokula plastiki

Wanasayansi wagundua viwavi wanaokula plastiki

Wanasayansi wagundua viwavi wanaokula plastiki

Viwavi wanaokula plastiki huenda wakawa utatuzi wa uchafuzi wa mazingira unaofanywa na plastiki kulingana na wanasayansi.

Waafiti katika chuo kikuu cha Cambridge wamegundua kwamba buu la nondo huyo ambalo linakula nta pia linaweza kula plastiki.

Utafiti umebaini kwamba mdudu huyo anaweza kuharibu mshikamano wa kikemikali wa plastiki vilevile anavyokula nta ya nyuki.

Kila mwaka,takriban tani milioni 80 za plastiki huzalishwa duniani.

Plastiki hizo hutumika kutengeza mifuko ya plastiki inayotumika katika maduka ya jumla kubebea bidhaa na inaweza kuchukua muda mrefu kuoza.

Viwavi wanaweza kuweka mashimo katika mifuko hiyo ya plastiki chini ya saa moja.

Hatahivyo viwavi wanaweza kuweka mashimo katika mifuko hiyo ya plastiki chini ya saa moja.

Daktari Paolo Bombeli ambaye ni mmoja ya watafiti anasema: Tutaanza na viwavi hao ,aliambia BBC.

”Tunahitaji kujua maelezo kuhusu vile viwavi hao wanavyofanya kazi.Tunahitaji kupata suluhu ili kuweza kupunguza plastiki”.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

barafu

Greenland: Wanakijiji wa Innaarsuit waondolewa karibu na donge kubwa la barafu

Donge kubwa la barafu lililopo katika maji limekaribia kijiji kimoja magharibi mwa Greenland na kusababisha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *