Home / Michezo / Mashabiki waichangia Yanga mil 9/-

Mashabiki waichangia Yanga mil 9/-

KLABU ya Yanga imeweka wazi makusanyo ya fedha za maendeleo kupitia mitandao ya simu ambapo ndani ya siku nne tangu waombe mashabiki na wanachama kuwachangia wamekusanya Sh milioni 9.6.

Mwanzoni mwa wiki hii, Yanga iliomba wanachama na mashabiki kuwachangia fedha baada ya kukiri kukabiliwa na ukata tangu kujiweka pembeni kwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji.

Akitoa taarifa za makusanyo hayo jana Katibu Mkuu, Charles Mkwasa alisema uchangiaji ulianza kwa kasi lakini kadiri siku zinavyokwenda hamasa inapungua. “Mungu awabariki wote wanaochangia.

Kama uongozi tunasisitiza fedha hizi zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa baada ya kukusanywa. Lakini angalizo kwetu idadi ya wachangiaji kutoka siku ya kwanza hadi sasa inashuka, hii ina maana hamasa kwa kiasi fulani imepungua,”alisema.

Alisema siku waliyotangaza kuchangiwa Aprili 24, mwaka huu mchana walipokea maingizo 642 na jumla ya makusanyo Sh 2,18,911. Siku iliyofuata walipokea maingizo 1181 na makusanyo Sh 4,248,751, siku ya tatu walipokea maingizo 625 na makusanyo Sh 2,296,966 na juzi walipokea maingizo 290 na makusanyo Sh 866,795.

Mkwasa aliwashukuru mashabiki na wanachama wa klabu hiyo na kuwaomba kuendelea na hamasa ya uchangiaji kwa akaunti maalumu ya selcom kupitia namba 150334. “Makusanyo haya yanafanyika kupitia mitandao ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money. Hakika mpaka sasa tunajivunia ushirikiano wenu na tunawaomba taarifa ya leo iwe chachu ya kufanya kikubwa zaidi,” alisema.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *