Home / Habari za Kimataifa / UN KATIKA JITIHADA ZA KUTATUA MZOZO WA KISIASA DRC

UN KATIKA JITIHADA ZA KUTATUA MZOZO WA KISIASA DRC

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wanazuru Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kujaribu kuzima mvutano wa kisiasa nchini humo.

Rais Joseph Kabila anamaliza muhula wake wa pili na wa mwisho mwezi ujao, lakini uchaguzi umehairishwa.

Upinzani unamtuhumu rais kwamba anachelewesha uchaguzi makusudi ili abaki madarakani.

Shirika la kutetea haki za binaadamu, Human Rights Watch, limeliomba Baraza la Usalama kumsihi Rais Kabila aondoke madarakani muhula wake ukimalizika, ili kuepusha msukosuko mkubwa zaidi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mtanzania mwanaharakati Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Rebeca Gyumi Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *