Home / Habari za Kimataifa / Msichana akataa kuolewa na makamanda wa Boko Haram

Msichana akataa kuolewa na makamanda wa Boko Haram

Msichana aliyekataa kuolewa na wapiganaji wa Boko Haram

Msichana wa miaka 14 aliyejisalimisha alipokuwa akitekeleza shambulio la kujitolea muhanga katika kambi ya jeshi kaskazini mwa jimbo la Maiduguri nchini Nigeria amesema aliteuliwa kutekeleza shambulio hilo kwa kukataa kuolewa na waasi wa Boko Haram.

Amesema alitekwa nyara na babake huko Gwoza, katika jimbo la Borno mwaka 2013, Shirika la habari la Nigeria limesema.

”Nimesalia kwa zaidi ya miaka mitatu katika mikono ya Boko Haram. Wafuasi watatu tofauti wa kundi hilo waliwasilisha ombi la kutaka kunioa lakini nikakataa.

Wawili kati yao walikuwa makamanda.

Nilipokataa kwa mara ya tatu , kamanda mmoja alikasirika na kunitishia kuniua mimi na babangu.

Nilimwambia heri nife kuliko kuolewa na waasi wa Boko Haram.”

”Baada ya wiki moja , wakasema kwa vile nimekataa kuolewa , ninastahili kupelekwa huko Maiduguri kutekeleza mauaji.Watatu wakanishika mikono yangu na wakanidunga sindano.”

Aliambia shirika la habari la Nigeria (NAM) kwamba baadaye alisafirishwa katika kambi ya jeshi pamoja na washambulizi wengine.

Mmoja wao alilipua bomu lake kwenye mkanda wake wa kifuani , lakini lilimua yeye mwenyewe, kwa upande wake mwengine, alisema alipigwa risasi na wanajeshi, Shirika la habari la Nigeria limeripoti.

Alisema hivyo na akatoa mkanda wake wa bomu na kujisalimisha.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *