Home / Habari za Kimataifa / Uchaguzi wa Kenya: Maswali muhimu na majibu

Uchaguzi wa Kenya: Maswali muhimu na majibu

Mpiga kura nchini Kenya

Kabla ya uchaguzi utakaofanyika nchini kenya mwezi Agosti, kuna baadhi ya maswali ambayo wengi wenu mmekuwa mkiuliza.

Tutakuwa tukiongezea masuali mapya katika ukurasa huu, kadiri siku zina

Wanasiasa wanachangisha vipi fedha za matumizi katika kampeni zao?

Kenya haina sheria za uchangishaji wa fedha za kampeni za uchaguzi.

Majaribio ya tume ya uchaguzi kuwasilisha bungeni mswada wa kudhibiti fedha za kampeni yalizimwa na wabunge.

Tume hiyo ilikuwa imetoa mapendekezo yafuatayo kwa viti tofauti.

  • Rais: $50m
  • Magavana: $4m
  • Wabunge na Maseneta: $290,000
  • Wawakilishi wa Wadi: $97,000

Kutokuwa na sheria hii kunamaana kuwa wagombeaji wana uhuru ya kutumia pesa vile wanavyotaka.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, “Mara nyingi fedha hizo hutumika kufanya mipango na kugharimia matangazo lakini wagombea wengi na vyama pia hutumia kuwahonga wapiga kura”.

Gazeti hilo liliripoti kuwa katika uchaguzi wa 2013, muungano wa upinzani wakati huo Cord, ulitumia zaidi ya $50m (£40m) huku mrengo unaotawala wa Jubilee ukitumia zaidi ya $100m kuendesha kampeni za urais.

Wanasiasa huchangisha pesa kutoka wafanyibiashara na wengine hufanya harambee. Vyama vya upinzani hata hivyo vimekuwa vikishutumu chama tawala kwa kutumia rasilimali za serikali katika kampeni.

Je, kutakuwepo na vita vya baada ya uchaguzi?

Ken Opalo, kutoka chuo kikuu cha Georgetown Marekani, anasema ijapokuwa kuna dalili za uwezekano wa kutokea kwa fujo, hali haitakuwa mbaya kama iliyoshuhudiwa miaka 10 iliyopita, wakati watu zaidi ya 1,000 walifariki dunia na 600,000 kufurushwa makwao.

“Sijali sana kuhusu uchaguzi mkuu. Hatua halisi itaonekana katika kaunti,” aliongeza.

“Vita kwa uhakika vitakuwepo. Lakini, sana sana itaonyesha picha ya hali halisi, kuliko kutokea kwa vita vikali na kufeli kwa serikali.

Huu ni mtazamo ambao umetolewa na Nic Cheeseman, Profesa wa demokrasia katika Chuo kikuu cha Birmingham Uingereza na mdadisi wa siasa za Kenya.

Anasema kuwa: “Mizozano katika uchaguzi wa mchujo katika vyama ni jambo la kutia tumbo joto. Lakini hazitaleta vurugu kubwa wakati wa uchaguzi mkuu wenyewe”.

Vurugu katika uchaguzi wa mchujo unatueleza ninikuhusu uchaguzi

Ni taswira gani ya uhakika kuhusu uchumi wa Kenya?

Kenya imedumisha ukuaji thabiti wa uchumi kwa miaka tano iliyopita, ambapo uchumi umekua kwa asilimia 5% kila mwaka.

Hata hivyo, kupanda kwa bei ya bidhaa za kawaida kama maziwa, mkate na unga vimesukuma juu mfumuko wa bei kwa asilimia 12%, na familia nyingi nchini Kenya wanasema kuwa wanateseka kimaisha.

Wakenya wamekuwa wakitumia kitambulisha mada #CostOfLivingKe (Gharama ya kuishi Kenya) kujadili kupanda bei za bidhaa za kawaida na jinsi wanavyobadilisha mitindo yao ya kuishi.

“Kila mwaka wa uchaguzi, uchumi pia huenda chini na hali ndiyo iyo hiyo mwaka huu huku wawekezaji wakingojea kuona jinsi uchaguzi utakavyoenda,” Kwame Owino, Mkurugenzi Mkuu katika taasisi ya masuala ya uchumi aliiambia BBC.

“Baadhi ya kampuni zinapunguza idadi ya wafanyakazi, sekta isiyo rasmi ikiwa mwajiri mkubwa,” aliongezea.

Mazuri:

Kenya ilipata uwekezaji wa jumla ya $1bn, baada ya kufanya mageuzi mbalimbali kama vile kama kupunguza kwa gharama ya kufanyia biashara na urasimu, uwekezaji katika miundombinu na kupunguzwa kwa gharama ya viza jambo ambalo limeimarisha utalii.

Mabaya:

Hata hivyo uchumi umekumbwa na kukita mizizi kwa utoaji wa rushwa, uhasama wa kisiasa na hatua ya serikali kudhibiti viwango vya riba – njia iliyokuwa ipunguze gharama ya mikopo lakini haijafanikiwa.

Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) linasema kuwa Kenya ina kiwango cha ukosefu wa ajira cha juu zaidi katika kanda hii, huku watu wanne kati ya kumi wakiwa hawana kazi.

Bw Owino anasema kuwa wapigaji kura ambao hawajaridhishwa na serikali wanaweza kuunga mkono wale wanaodhania watajali mahitaji yao ya kiuchumi.

Ufisadi ni mbaya kiasi gani?

Katika ripoti yake ya 2016, shirika la Transparency International liliweka Kenya katika nafasi ya 145 kati ya nchi 176 kwa kukithiri kwa rushwa.

Ililaumu nafasi hiyo chini ya Kenya kwa uzembe na kukosa ufanisi wa mashirika ya kupambana na ufisadi, ikisema kukosa kuadhibu waliopatikana wakishiriki katika ulaji rushwa kumekuwa kikwazo kikubwa.

Mwanaharakati wa kupambana na ufisadi John Githongo ameitaja serikali ya rais Uhuru Kenyatta kama “iliyo na ufisadi mkubwa katika historia ya Kenya”.

Rais Kenyatta hata hivyo amesema kuwa juhudi zake za kupambana na ufisadi zinadhoofishwa na mahakama, ambayo inashughulikia kesi hizo kwa mwendo wa kinyonga, na kulitaja shirika na kupambana na ufisadi kuwa vivu mno.

Bw Githongo alitaja ripoti kadhaa za kashfa inayoshirikisha madai ya kupandishwa kwa bei ya miradi na malipo kwa kampuni hewa.

Mwakani 2015, Kenyatta aliwasimamisha kazi na hatimaye kuwatoa ofisini mawaziri watano na maafisa wa juu serikalini kwa madai ya ufisadi.

Waziri mmoja alijiuzulu baada ya shinikizo kutoka kwa umma.

Wanachama wa upinzani pia wametajwa katika kashfa kadhaa, lakini wengine wameilaumu serikali kwa kuwasingizia.

Mashirika ya kikatiba yaliyobuniwa kupambana na ufisadi yameshutumiwa kuwa hawana msimamo wao binafsi.

Mdadisi wa masuala ya siasa nchini Kenya Barrack Muluka anawalaumu Wakenya wa kawaida kwa tatizo katika kukabiliana na ufisadi, akisema kuwa wamefumbwa macho na ukabila: “Serikali yaweza kuiba itakavyo na Wakenya watafurahia ikiwa tu ni “wezi wetu.”

Aligusia uchaguzi wa mchujo mwezi Aprili ambapo wagombeaji waliokuwa na utata kuhusu uadilifu wao na wale waliodaiwa kushiriki katika ufisadi bado walishinda uchaguzi wa mchujo.

Bw Githongo anaitaja hatua hiyo kuwa sawa na ” kuhalalisha upuuzi”

Anasema kuwa wizi umekuwa jambo la kawaida: “Wale tuliowaita wezi sasa ni watu waliopambana na kufanikiwa maishani.”

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *