Home / Habari Za Kitaifa / TBS yashauri vyuo vikuu kuanzisha kozi ya ugezi

TBS yashauri vyuo vikuu kuanzisha kozi ya ugezi

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mwito kwa vyuo vya elimu ya juu nchini kuanzisha kozi ya ugezi, ili kuzalisha wataalamu wa kutosha wa fani hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Profesa Egid Mubofu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Tumaini Mtitu, alisema kuna uhaba mkubwa wa wataalamu wa ugezi katika shirika hilo, changamoto itakayoweza kutatuliwa kwa kuzalishwa wataalamu wa ugezi wa kutosha katika vyuo vilivyopo nchini.

Alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ugezi Duniani. Kwa mujibu wa Mtitu, changamoto ya uhaba wa wataalamu wa ugezi inalifanya shirika hilo kulazimika kuwatumia wagezi wachache waliopo, hivyo kuwapa wakati mgumu.

Mtitu alisema kuwa chuo pekee ambacho kimekuwa kikitoa mafunzo ya ugezi ni cha Utawala wa Biashara (CBE), ambacho awali kilikuwa kinatoa wataalamu katika ngazi ya Stashahada na kwa sasa kimeanza kutoa shahada ya kwanza ya ugezi.

Alisema shirika hilo linakabiliwa na changamoto nyingine ya uhaba wa vifaa vya kisasa vya ugezi kutokana na kukosa fedha za kutosha kuvinunua kwa wakati. Hata hivyo, Mtitu alisema waliamua kutenga bajeti kwa ajili hiyo.

Changamoto nyingine aliyoitaja ni miundombinu ya maabara ya ugezi kutoruhusu upanuzi wa nyanja za ugezi, akisema kuwa ilijengwa mwaka 1982 hivyo kutoendana na mahitaji ya sasa.

Mbali na hayo, Mtitu aliwataka wadau mbalimbali katika sekta ya usafirishaji, taasisi binafsi na mamlaka za serikali zinazohusika na usafiishaji, kuhakikisha vifaa vyote vinavyotumika katika sekta hiyo vinafanyiwa ugezi, kwa sababu usahihi wa vipimo huleta ubora na usalama wa huduma.

Tanzania ni nchi ya nne Afrika inayotambuliwa kwa kuwa na maabara ya ugezi mahiri ikifuata baada ya nchi za Kenya, Misri, na Afrika Kusini.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *