Home / Habari Za Kitaifa / Mwenyekiti Bodaboda Shinyanga ajinyonga

Mwenyekiti Bodaboda Shinyanga ajinyonga

MWENYEKITI wa Chama cha Waendeshaji Bodoboda mkoani Shinyanga, Jacob Paulo amekutwa amekufa.

Inadaiwa amekufa kwa kujinyonga, baada ya kutuhumiwa na wenzake kuwa anawasaliti kwa askari wa Jeshi la Polisi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Jumanne Mulilo, amethibitisha kuwapo kutokea tukio hilo jana mchana nyumbani kwake katika Mtaa wa Mwinamila, Kata ya Ngokoro, Manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa mke wa marehemu Rebeca Amosi na jirani yake, Sarah Edward, Mwenyekiti huyo (Jacob) alifikia uamuzi huo baada ya kukerwa na tuhuma na vitisho kutoka kwa waendesha bodaboda wenzake waliodai anawasaliti kwa kutoa taarifa zao kwa Jeshi la Polisi na kuwafanya wakamatwe wanapofanya uhalifu.

Naye Sarah ambaye ni jirani alisema baada ya mke wa marehemu kumjulisha kuhusu ujumbe za vitisho anazotumiwa mumewe kutoka simu mbalimbali, alimshauri amhimize mumewe kujivua uongozi, lakini akasema mumewe atachukua hatua hiyo.

Gazeti hili lilishuhudia polisi wakiuondoa mwili wa marehemu kuupeleka Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Diwani wa Kata ya Ngokoro, Emmanuel Ntobi alithibitisha tukio hilo na kutaka iundwe kamati maalumu kuchunguza tukio la vurugu za bodoboda katika

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *