Home / Habari Za Kitaifa / Yatima waomba mke wa Rais awasaidie kupata kiwanja

Yatima waomba mke wa Rais awasaidie kupata kiwanja

KITUO cha kulea yatima cha Hiari kilichopo Chang’ombe Dar es Salaam, kimemuomba mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli akisaidie kupata eneo kutokana na walilonalo kuwa finyu.

Kiongozi na mlezi wa kituo hicho, Aminajat Kilemia alitoa maombi hayo juzi wakati akizungumza na =gazeti hili Ikulu, Dar es Salaam baada ya kupokea msaada wa vyakula vya futari kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan na sikukuu ya Idd el Fitr.

Msaada huo ulitolewa na Mama Janeth kwa vikundi vinane vinavyolea yatima na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi Dar es Salaam. Msaada ulihusisha kilo 2000 za sukari, kilo 2000 za mchele na tende kilo 800 ukiwalenga watoto 700 katika vituo hivyo.

Pamoja na shukrani hizo, Kilemia alimuomba Mama Janeth kuwasaidia kupata eneo la kujenga kituo kikubwa cha kulea watoto hao yatima kutokana na eneo waliloko sasa, kuwa dogo. Kwa sasa kituo hicho kina watoto 62 wenye umri kuanzia umri miaka sifuri hadi wa umri wa vyuo vya elimu ya juu.

Alisema wana uhitaji wa eneo la ukubwa wa kuanzia heka tatu ili kujenga kituo, kulima bustani za mboga na sehemu ya michezo kwa watoto. Kwa mujibu wa mlezi huyo, idadi ya watoto katika kituo hicho imekuwa ikiongezeka kutokana na watoto hao kuletwa kutoka Idara ya Ustawi wa jamii na Polisi.

Alisema wapo wanaosoma Sekondari ya Azania na huwalipia hosteli ya Sh 130,000 kwa mwezi na wa sekondari ya Tambaza wako wanne kila mmoja ni Sh 110,000 kwa mwezi na hali hiyo inatokana na ufinyu wa nyumba ya kituo hicho. Alisema wapo wanafunzi watatu katika Chuo Kikuu cha St Joseph, Kibamba na huwalipia Sh 50,000 kwa mwezi kukaa hosteli.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *