Home / Habari Za Kitaifa / Idd el- Fitr kuswaliwa Moshi, Majaliwa mgeni Baraza la Idd

Idd el- Fitr kuswaliwa Moshi, Majaliwa mgeni Baraza la Idd

BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), limesema Sikukuu ya Idd el-Fitr kitaifa itaswaliwa Moshi mkoani Kilimanjaro, Juni 25 au 26 kutegemea na mwandamo wa mwezi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Bakwata, Salim Abeid, swala ya Idd el-Fitr itaswaliwa kwenye Uwanja wa Chui mbele ya Shule ya Msingi Mwenge kuanzia saa 1.30 asubuhi.

Katibu Mkuu wa Bakwata alisema swala hiyo itafuatiwa na Baraza la Idd litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Polisi (CCP) Moshi baada ya swala ya Adhuhuri.

Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na pia watakuwepo viongozi mbalimbali. Waislamu nchini kila mwaka hujumuika na wenzao duniani kusherehekea sikukuu hiyo baada ya kumaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *