Home / Habari za Kimataifa / Marufuku ya usafiri kwa mataifa sita ya Kiislamu yatekelezwa Marekani

Marufuku ya usafiri kwa mataifa sita ya Kiislamu yatekelezwa Marekani

Maandamano ya kupinga marufuku ya rais Trump yafanyika Marekani

Raia kutoka mataifa sita ya kiislamu na wakimbizi wote sasa wanakabiliwa na masharti magumu ya kuingia nchini Marekani kufuatia marufuku ya rais Trump ambayo imezua utata.

Hii inamaanisha kwamba watu wasio na uhusiano wa karibu na wale wanaoishi Marekani ama uhusiano wa kibiashara nchini Marekani huenda wakanyimwa Visa na kuzuiliwa kuingia.

Bibi, shangazi, mjomba ,binamu na mpwa hawakubaliki kuwa watu wenye uhusiano wa karibu na mtu anayetaka kuingia taifa hilo.

Sheria hiyo itawaathiri raia wanaoishi Iran, Syria, Somalia, Sudan na Yemen pamoja na wakimbizi wote.

Muda mfupi kabla ya marufuku hiyo, ilibainika kwamba jimbo la Hawaii lilikuwa limemuuliza jaji mmoja wa kijimbo kufafanua sheria hiyo.

Jimbo hilo awali limekuwa likiishutumu serikali ya Marekani kwa kukiuka sheria ya mahakama ya juu kupitia kuwatenga watu.

Kuzuia raia wa baadhi ya nchi za kiislam ilikua moja ya ajenda za Trump wakati wa kampeni za urais

Mapema wiki hii, mahakama ya juu ilikubali marufuku hiyo kutimizwa kwa muda hatua iliositisha sheria iliowasilishwa mahakamani kuzuia sera hiyo muhimu ya Trump.

Mahakama iliamuru kwamba watu wanaotafuta Visa kuingia Marekani kutoka mataifa hayo sita pamoja na wakimbizi wote, watalazimika kuthibitisha kuwa na uhusiano wa karibu na raia wa taifa hilo .

Mahakama ya juu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu marufuku hiyo mnamo mwezi Oktoba.

Kulingana na sheria hiyo mpya, katika kipindi cha siku 90 zijazo raia kutoka mataifa hayo sita wasio na uhusiano wa karibu na raia wa Marekani hawataruhusiwa kuingia nchini humo.

Wale watakaoruhusiwa ni wale walio na wazazi wao, mke au mume, mtoto wa kiume ama wa kike na mwana wa kambo.

Pia wale wasio na uhusiano wa kibiashara au ule wa masomo na Marekani hawataruhusiwa kuingia.

Hatahivyo maelezo hayo yanasema kuwa uhusiano huo ni sharti uwe kwa njia rasmi, ulionakiliwa na sio kwa lengo la kukwepa agizo hilo.

Wale walio na Visa hawataathiriwa.Wale wenye uraia wa mataifa mawili wanaotumia pasipoti zao pia wataruhusiwa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *