Home / Habari za Kimataifa / Putin aagiza wanadiplomasia 755 wa Marekani kuondoka Urusi

Putin aagiza wanadiplomasia 755 wa Marekani kuondoka Urusi

Kufukuzwa wa wanadiplomasia hao kutapunguza idadi hadi 455

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu.

Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.

Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo

Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo.

Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.

Urusi imewapiga wanadiplomasia wa Marekani

Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.

Akizungumza na wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.

Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kupata ushindi.

Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.

Urusi inalitwaa ghala hili la Marekani lililo Moscow

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *