Home / Habari za Kimataifa / Marekani imemuwekea Rais Maduro vikwazo

Marekani imemuwekea Rais Maduro vikwazo

Marekani imezuia mali za rais Nicolas Maduro anazomiliki Marekani

Marekani imeidhinisha vikwazo dhidi ya rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.

Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi uliokumbwa na mzozo Venezuela, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa taarifa kutishia kumchukulia kiongozi wa taifa hilo hatua nzito na za haraka.

Imezuia mali zote anazomiliki Maduro Marekani na waziri wa fedha Marekani, Steven Mnuchin amemtaja Maduro kuwa dikteta.

“Uchaguzi wa jana wa haramu unathibitisha Maduro ni dikteta asiyezingatia matakwa ya raia wa Venezuela”, alisema katika taarifa yake.

Hii sio mara ya kwanza hatua zimechukuliwa dhidi ya viongozi wa serikali , huku viongozi wakuu 13 wa utawala wa Maduro wakilengwa kwa vikwazo kama hivyo wiki iliopita.

Mtihani mkubwa hatahivyo utajiri iwapo Washington itaamua kuidhinisha vikwazo vya nishati dhidi ya tifa hilo mzalishaji mafuta.

Wengi wanahofia hatua ya aina hiyo itaathiri vibaya uchumi, na hivyo kuwaathiri raia maskini katika taifa hilo kuliko walio katika utawala.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mtanzania mwanaharakati Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Rebeca Gyumi Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *