Home / Habari Za Kitaifa / Ummy awapongeza Rukwa kudhibiti vifo vya wajawazito

Ummy awapongeza Rukwa kudhibiti vifo vya wajawazito

SERIKALI imesema inaendelea kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto ili wajawazito wanaohudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vinavyotoa huduma ya afya 2020.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu mjini Nkasi akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa wa Rukwa. Alisema wajawazito wanaohudhuria na kujifungulia kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya imefikia asilimia 95 huku kitaifa ikiwa asilimia 64.

“Niwapongezeni Rukwa maana tayari mmefikia asilimia 95 ya wajawazito wanaojifungulia katika vituo vinavyotoa huduma za afya hata kabla ya 2020 hongereni sana ndio maana vifo vya wajawazito mkoani hapa vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi viko chini,” alisema.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Boniface Maganga alimueleza Waziri Mwalimu kuwa vituo 214 kati ya 223 vilivyopo mkoani humo vinatoa huduma muhimu ya uzazi na mtoto ambapo wajawazito 161,089 walihudhuria kliniki mwaka 2016.

Aliongeza kuwa katika kipindi hicho wajawazito 43, 938 kati yao 41,698 ikiwa ni sawa na asilimia 95 walijifungulia katika vituo vinavyotoa huduma ya afya ambapo 2,240 sawa na asilimia 15 walijifungulia nje ya vituo hivyo. Aidha, watoto wapatao 47,268 wenye umri chini ya mwaka mmoja walipatiwa chanjo ikiwa ni asilimia 93 ya watoto 50,728 waliotarajiwa kupewa chanjo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *