Home / Habari za Kimataifa / TRUMP AJITOKEZA KWA KUSTUKIZA MGAHAWANI NEW YORK

TRUMP AJITOKEZA KWA KUSTUKIZA MGAHAWANI NEW YORK

Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliwashangaza wateja, na wanahabari wanaofuatilia safari zake, baada ya kujitokeza kwa kushtukiza katika mgahawa mmoja New York.

Wanahabari waliopewa kazi ya kufuatilia safari zake walibaki kushangaa kwani walikuwa wameelezwa kwamba angesalia nyumbani jioni hiyo.

Lakini badala yake, aliandamana na kundi ndogo la maafisa hadi kwenye mgawaha wa 21 Club katika mtaa wa Manhattan, mmoja wa migahawa anayoipenda sana.

Watakaoumia na watakaofaidi chini ya Trump Marekani

Video zilizopigwa wakati wa kisa hicho Jumatano zinamuonyesha Bw Trump akiwasalimia wateja na kuwaambia kwamba atapunguza kodi wanayolipa kwa serikali.

Kuwasili kwake 21 Club kulijulikana baada ya mwandishi wa Bloomberg, Taylor Riggs, ambaye kibahati alikuwa ameenda kwenye mgahawa huo, alipakia kwenye Twitter ujumbe wa kusema kwamba Trump alikuwa amefika kwenye mgahawa huo. Hata hivyo, alikosea jina la eneo na badala yake akasema ilikuwa ni Keene. SOURCE BBC SWAHILI

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *