Home / Habari za Kimataifa / Wabunge wapya wakataa kupunguziwa mishahara Kenya

Wabunge wapya wakataa kupunguziwa mishahara Kenya

Wabunge katika bunge la Kenya

Baadhi ya wabunge wapya nchini Kenya wamepinga mpango wa kupunguza mishahara yao kwa asilimia 15 kulingana na chapisho la mtandao wa Twitter wa chombo kimoja cha runinga.

Hatua ya kupunguza mshahara huo inayoshirikisha marupurupu kadhaa ilitarajiwa kuanza kutekelezwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti nane.

Mnamo mwezi Juni, tume ya marupurupu na mishahara ilisema kuwa mpango huo ulilenga kupunguza mishahara ya wafanyikazi wa serikali kwa asilimia 35.

Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wavunge wanaolipwa mishahara ya juu duniani, na hatua ya kuipunguza mishahara hiyo ni mojwapo ya mipango ya serikali kupunguza mishahara ya wafanyikazi wa serikali.

Mapato ya wastani nchini Kenya ni dola 150 kwa mwezi..

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *