Home / Habari za Kimataifa / Baraza la usalama la UN laionya Korea Kaskazini

Baraza la usalama la UN laionya Korea Kaskazini

Kombora la Korea kaskazini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza.

Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini.

Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia.

◾Baraza la Usalama la UN lailaani Korea Kaskazini
◾UN yatishia kuichukulia hatua Korea Kaskazini
◾Korea Kaskazini yawaachilia raia wa Malaysia
◾Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu

Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo.

Majeshi ya Korea Kusini na Marekani yamekuwa yakifanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea Kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *