Home / Habari za Kimataifa / Msichana ashambuliwa na panya Ufaransa

Msichana ashambuliwa na panya Ufaransa

Msichana wa umri wa miaka 14 ambaye ana ulemavu amelazwa hospitalini Ufaransa akiwa na vidonda vilivyotokana na kushambuliwa na panya chumbani mwake kaskazini mwa Ufaransa.
Msichana huyo ako hali mahututi.
Taarifa zinasema msichana huyo alikuwa amelala katika ghorofa ya kwanza aliposhambuliwa na panya wengi katika chumba cha kukodishwa Roubaix.
Mtaalamu wa matibabu aliyenukuliwa na jarida la France Info alisema msichana huyo ana vindonda 45 usoni, 150 mikononi na 30 miguuni.
Babake msichana huyo amemshtaki landilodi kwa utepetevu.
Taarifa zinasema jaa la taka lilikuwa limejaa taka.
Paris kukabiliana na ongezeko la panya
Mashabiki wamrushia panya mchezaji nchini Denmark
Panya asababisha safari ya ndege kuchelewa Uingereza
Panya wavamia na kuharibu afisi ya rais Buhari Nigeria
Mwanamume huyo, ambaye ana watoto wengine wawili, anasema alimpata msichana huyo wake mlemavu kwa jina Samantha akiwa “amevunja damu sana” kitandani Jumamosi.
Anasema msichana huyo alikuwa buheri wa afya familia hiyo ilipoenda kulala. Yeye na watoto hao wengine walikuwa wanalala ghorofa za juu.
Baadhi ya alama za vidole kwenye vidole vya msichana huyo vimefutika na madaktari hawawezi kumtibu kwa njia ambayo zitarejea.
Familia hiyo imehamia nyumba nyingine na polisi wanaendelea na uchunguzi.
Msichana huyo amechunguzwa kubaini iwapo aliambukizwa maradhi, yakiwemo kichaa cha mbwa. Hata hivyo hakupatikana ameambukizwa kichaa cha mbwa.
Visa vya panya kuwashambulia binadamu ni nadra sana, lakini panya wakiwa na njaa sana hula maiti.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *