Home / Habari za Kimataifa / Wadau wa vyombo vya habari wakutana Tanzania

Wadau wa vyombo vya habari wakutana Tanzania

Washiriki katika mkutano
Wadau mbalimbali wa vyombo vya habari na taasisi za kiraia nchini Tanzania wanakutana Alhamisi jijini Dar Es Salaam kujadili kanuni za maudhui ya mitandaoni.
Mkutano huo ambao umefunguliwa rasmi na katibu mkuu wa wizara ya habari nchini Tanzania pia umehudhuriwa na wakurugenzi mbali mbali kutoka serikalini.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, katibu mkuu wa wizara prof. Elisante Ole Gabriel amesema, kutokana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya mtandao, wakati umefika kuboresha kanuni za maudhui ya mtandaoni kwa lengo la kusaidia tasnia na wala sio kudhibiti.
Mitandao ya kijamii ilivyotumiwa uchaguzi mkuu Kenya 2017
Wahariri Tanzania kususia habari za Makonda
Tanzania: Waziri aomba subira ripoti ya Clouds
Ameongeza kusema lengo la kuwashirikisha wadau mbalimbali ni kuepuka kutunga kanuni ambazo baadae zitakinzana na utendaji kazi.
Miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wa siku moja ni ma bloga, wamiliki wa mitandao na waandishi wa habari.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *