Home / Habari Za Kitaifa / Wanunuzi wa tumbaku marufuku kutumia dola

Wanunuzi wa tumbaku marufuku kutumia dola

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ameagiza wanunuzi wa tumbaku wilayani Chunya kuacha kutumia mfumo wa malipo kwa Dola za Marekani, badala yake watumie shilingi za kitanzania.

Makalla amesema kupitia mfumo wa malipo kwa dola wapo wajanja ambao wamekuwa wakinufaika kwa kuwaibia wakulima wasiokuwa na uelewa wa kutosha juu ya ubadilishaji fedha kimahesabu.

Katika kikao chake na wadau wa zao la Tumbaku kilichofanyika katika kijiji cha Lupatingatinga, alisema kuendelezwa kwa misamiati ya dola kutasababisha baadhi ya wakulima kuendelea kunyonywa huku wajanja wachache wakineemeka kwa jasho la wanyonge.

“Kuna viongozi siyo waadilifu wanawapiga wananchi kupitia dola, siyo watu wote wana elimu ya ubadilishaji fedha. Tukiendeleza dola tutatoa mwanya kwa wapigaji, acheni misamiati ya dola wewe njoo na shilingi kama unakwenda kuuza kwa dola huko utajua wewe hiyo ibaki siri yake,” alisisitiza.

Wakati huo huo, Makalla alisema atatuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kukagua matumizi ya fedha za Mfuko wa Kuendeleza Elimu wilaya ya Chunya (Chudetu) ambazo zimekuwa zikikusanywa kutoka kwa wakulima wa zao la tumbaku pekee huku wadau wengine wakiachwa.

Alisema iwapo Halmashauri inakiri fedha hizo hapo awali zilisaidia ujenzi wa shule za kata na maabara za sekondari, lazima sasa itambulike zinazokusanywa kwa sasa zinapelekwa wapi wakati serikali inatekeleza Sera ya elimu bure.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *