Home / Habari Za Kitaifa / Mbwa 400, paka 20 wachanjwa Kahama

Mbwa 400, paka 20 wachanjwa Kahama

HALMASHAURI ya Mji wa Kahama imeadhimisha Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za Wanyama (Tapo) kwa kutoa chanjo kwa mbwa 419 na paka 20.

Akizungumza katika maadhimisho hayo mwishoni mwa juma, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanyama nchini, Yohana Kashililah, alisema wameamua kuadhimisha siku hiyo ambayo hufanyika kila Septemba 28 kila mwaka, kwa kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa na paka katika Halmashauri ya mji wa Kahama.

Kashililah alisema utoaji huo wa chanjo utafanyika kwa siku tatu mfululizo na kuongeza kuwa kujikinga na kichaa cha mbwa sio kumuua mnyama, bali ni kutoa kinga kwa mnyama husika.

Alisema shirika lake limepanga ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa kichaa cha mbwa uwe umetokomezwa nchini kupitia chanjo na utoaji elimu kwa wafugaji wa wanayama hao.

Alisema kwa siku hizo utoaji chanjo umelenga kuwafikia mbwa 600 hadi 800 na kwamba juzi pekee, walichanja mbwa 419 na paka 20. Ofisa mifugo kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama, Kija Daudi alisema kuwa siku za nyuma Halmashauri ilikuwa ikishindwa kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa kutokana na ukosefu wa pesa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

wakulima tanzania

Wakulima Tanzania watafuta masuluhisho kwa changamoto zao

Wakulima nchini Tanzania wameonya kuwa huenda nchi hiyo ikaingia kwenye baa la njaa kutokana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *