Home / Habari Za Kitaifa / Tanzania kinara malipo mtandaoni

Tanzania kinara malipo mtandaoni

TAASISI ya Trademark East Africa imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania kuwa ndiyo nchi inayoongoza nchi zote za Afrika Mashariki kwa matumizi ya mifumo ya malipo kwa njia ya mtandao, kulipia huduma mbalimbali za kibiashara, hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara.

Aidha, hatua hiyo imeifanya Tanzania kuwa ni nchi ya mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara. Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi ambaye alisema kupitia ufadhili wa TradeMark East Africa (TMEA), kwa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo cha Tanzania (TCCIA) na kile cha Zanzibar (ZNCCIA), kumeifanya Tanzania kuwa ndiyo nchi ya kwanza kunufaika na kufaidika na mfumo madhubuti na wa kisasa wa usajili vyeti vya uhalisia na kuripoti vikwazo vya kibiashara kwa kutumia simu za mkononi.

Mbilinyi aliyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Malipo kwa njia ya Mtandao kwa TCCIA ujulikanao kwa jina la Lipa Fasta uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga alisema, TMEA imetumia zaidi ya Dola za Marekani 600,000 katika kufanikisha mradi huu kwa TCCIA, lakini pia unahusisha ZNCCIA, fedha za kugharimia mpango huu, zimetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (DFID) kupitia Trade- Mark, East Africa (TMEA) inayosimamia utekelezaji wa mradi huo. Kwa upande wake, Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja alisema, “Tunaishukuru sana TMEA kwa misaada wa kugharimia mfumo huu muhimu ambao utaokoa muda na kupunguza gharama”.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

wakulima tanzania

Wakulima Tanzania watafuta masuluhisho kwa changamoto zao

Wakulima nchini Tanzania wameonya kuwa huenda nchi hiyo ikaingia kwenye baa la njaa kutokana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *