Home / Michezo / Tetesi za soka Ulaya Jumanne 03.10.2017

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 03.10.2017

Alexi Sanchez wa Arsenal
Wachezaji wa Everton wanadhani kwamba mkufunzi Ronald Koeman anasubiri kufutwa kazi na mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri baada ya klabu hiyo kuanza msimu wake kwa mguu mbaya (Sun)
Arsenal wanataka kubadilishana mshambuliaji Alexis Sanchez na winga wa PSG Julian Draxler mnamo mwezi Januari (Daily Star)

Julian Draxler wa PSG kuingi Arsenal huku Alexis Sanchez akijiunga na PSG
Celtic inafaa kusubiri maombi ya mshambuliaji Leigh Griffiths, 27, kutoka kwa vilabu vingi vya Ligi ya Uingereza kulingana na naibu mkufunzi wa Scotland Mark McGhee. (Edinburgh News)
Inter Milan wanamtaka kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, ijapokuwa hawatarajii kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mnamo mwezi Januari (Premium Sport, via ESPN)
Wakati huohuo Manchester United itamwania kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil mnamo mwezi Januari huku mazungumzo yake ya kandarasi mpya Arsenal yakiendelea kukwama.. (Independent)

Mesut Ozil kuuzwa na Arsenal
Lakini Arsenal inaonekana kutaka kumuuza mchezaji huyo wa Ujerumani badala ya kumuachilia bure msimu ujao. (Daily Mirror)
Mshambualiji wa Arsenal Alexandre Lacazette anasema kuwa atam’bembeleza mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezman , 26, kujiunga na The Gunners msimu ujao.. (Match of the Day magazine, via Daily Telegraph)
Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka, huku Barcelona ikishindwa kuwasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata
Chelsea inahofu kwamba mshambuliaji wake mahiri aliyenunuliwa kwa £70m Alvaro Morata, 24, atakuwa nje kwa takriban mwezi mmoja akiwa na jeraha la nyonga.(Daily Mail)
Bodi ya West Ham bado inamuunga mkono kocha Slaven Bilic, licha ya uvumi unaoendelea kuhusu hatma yake ya siku zijazo. (London Evening Standard)
Beki wa Juventus Giorgio Chiellini, 33, anatarajiwa kutia saini kandarasi mpya licha ya kuhitajiwa na Chelsea. (Calciomercato)

Manchester United na Chelsea zinamsaka beki wa kati wa klabu ya Middlesbrough’s, 20, na mchezaji wa vijana wasiozidi miaka 21 katika timu ya Uingereza Dael Fry. (Teamtalk)
Manchester United na Chelsea zinamsaka beki wa kati wa klabu ya Middlesbrough’s, 20, na mchezaji wa vijana wasiozidi miaka 21 katika timu ya Uingereza Dael Fry. (Teamtalk)
Ajenti wa klabu ya Manchester United anamsaka Krepin Diatta, 18, ambaye anasema kuwa kiungo huyo wa klabu ya Sarpsborg hayuko tayari kuhamia kwa klabu kubwa ya Ulaya (FootMercato, via Metro)
Wamiliki wa klabu ya Birmingham City wameapa kumuunga mkono mkufunzi mpya Steve Cotterill kwa kuwasajili wachezaji wapya huku wakilenga kupanda juu ya ligi. (Birmingham Mail)

Dele Alli kushoto na kocha Southgate
Southgate atamsisitizia Dele Alli umuhimu wa kuwa na nidhamu baada ya mchezaji huyo, 21, kutoka Tottenham kupigwa marufuku ya kutocheza mechi moja kufuatia ishara yake ya kuonyesha kidole cha kati wakati wa mechi ya ushindi dhidi ya Slovakia mwezi uliopita(Daily Mail)
Mshambualiji wa Itali Simone Zaza, 26, alifanya makosa makubwa kwa kukubali kujiunga na West Ham amesema babake na ajenti wake.(Calciomercato)

Carlo Ancelotti
Carlo Ancelotti anasema kuwa atachukua likizo ya miezi 10 kabla ya kuamua kurudi katika ukufunzi wa soka baada ya kufutwa na Bayern Munich wiki iliopita (Gazzetta dello Sport)
Wakati huohuo , wachezaji wa Bayern Munich walifanya mazoezi kwa siri bila kocha huyo wa Itali.(Kicker)
Kiungo wa kati wa Tottenham Moussa Sissoko, 28, amepongezwa na meneja wa Ufaransa Didier Deschamps baada ya kuimarisha mchezo wake (London Evening Standard)

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *